Mchezo wa watani wa jadi November 7, 2020

Nyandajr10

New Member
Joined
Nov 5, 2020
Posts
2
Reaction score
5
Naam Hatimae November 7 iliyosubiriwa kwa muda mrefu Hatimae imewadia ni mechi kubwa inayobeba hisia za wapenda michezo wote nchini pamoja barani Africa kwa ujumla.

📍Ni mchezo wa nne unakutanisha timu hizi katika mwaka huu wa 2020

Kwa Mara ya kwanza mwaka huu timu hizi zilikutana January 4 kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya magoli 2-2
Shukran kwa magoli ya Meddie Kagere na Deo Kanda kwa upande wa simba na Balama mapinduzi &Banka kwa upande wa Yanga.

🔧Wachezaji wote waliofunga magoli kwenye mchezo huu wa January 4 hawatakuwepo kwenye mchezo wa Leo
📍Mchezo mwingine ulikuwa March 8 mchezo uliomalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0
Shukran kwa goli la wakili msomi Bernard Morrison.

Mchezo huu ulishuhudiwa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt Jonh pombe magufuli
📍Mchezo mwingine ulikuwa ni nusu fainal ya kombe la shirikisho Ambapo Yanga alipasuka goli 4-1
⚽Fraga
⚽Chama
⚽Miquisone
⚽Mzamiru
🔧Mpaka sasa kocha wa Simba Sven Van De broek ameiongoza Simba kwenye michezo mitatu dhidi ya Yanga
✅ Ushindi 1
❌Kufungwa 1
Draw 1
Huku kocha wa Yanga Cedric Kaze akitarajiwa kuongoza Yanga kwenye mechi yake na Simba kwa Mara ya kwanza

🔧Wachezaji wa kuchungwa Sana kwenye mchezo wa Leo kwa upande wa simba ni Luis Miquisone na Clatous Chama
Huku kwa upande wa yanga ni Farid Mussa na Mukoko Tonombe

🔧Mechi hii itakayochezwa majira ya saa 11 jioni itachezeshwa na waamuzi 6 huku mwamuzi wa Kati akiwa Elly Sassii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…