Mchezo wa Yanga na Waarabu

Mchezo wa Yanga na Waarabu

koryo

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
639
Reaction score
278
Jana nimebahatika kuuona mchezo wa Yanga na Waarabu kupitia luninga. Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa kweli Yanga wanatakiwa wakaze buti vinginevyo wataambulia patupu. Jana wale Waarabu walitawala uwanja mzima na walikuwa wananacheza kama wanavyotaka. Pasi za Yanga hazikuwa maakini kabisa. Kwa siku hizi zilizobaki mfanye masahihisho makubwa. Lugha ya kuwa Waarabu hawachomoki ilikuwa ni danganya toto.
 
ni kweli, lakini yanga wamejitahidi sana kimchezo kuliko huko siku za nyuma, tunaamini kwa serikali hii ya magufuli taasisi za kiserikali zitafanya vyema, serikali imara hufanya nchi iwe imara katika sekta zote, hongereni yanga
 
Waarabu ndiyo timu gani?
Hili ndio kosa linalofanyika hata kwa waandishi wa habari na magazeti,na watangazaji wa TV,hawataji jina ya hizi timu za nchi za kiarabu ,wala nchi zao,wanasema waarabu,wakati huko kwa waarabu kuna nchi nyingi na timu nyingi tofauti tofauti.
 
Kabisa mkuu. Kuna Morocco, Algeria, Libya, Misri, Tunisia. Wote hao ni waarabu wa nchi tofauti.
 
Jana nimebahatika kuuona mchezo wa Yanga na Waarabu kupitia luninga. Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa kweli Yanga wanatakiwa wakaze buti vinginevyo wataambulia patupu. Jana wale Waarabu walitawala uwanja mzima na walikuwa wananacheza kama wanavyotaka. Pasi za Yanga hazikuwa maakini kabisa. Kwa siku hizi zilizobaki mfanye masahihisho makubwa. Lugha ya kuwa Waarabu hawachomoki ilikuwa ni danganya toto.
Aliye sama waarabu hawachomoki hayuko hata kwenye benchi la ufundi la Yanga ni mhuni fulani asiyejua chochote kuhusu mpira ni mwanasiasa tuu huyo Murro mpira hata ukiingia ndani kwa bahati mbaya unavunja kila kitu asweze hata kuutuliza labda uwe na mkiaa!
Ushauri hao wasemaji na watendaji wa timu zetu wawe watu wa mpira! Siyo hawa wasioeleweka hata fani yao ni ipi!
 
ni kweli, lakini yanga wamejitahidi sana kimchezo kuliko huko siku za nyuma, tunaamini kwa serikali hii ya magufuli taasisi za kiserikali zitafanya vyema, serikali imara hufanya nchi iwe imara katika sekta zote, hongereni yanga
Mkuu hongera kwa kusema ukweli kuwa Yanga ni taasisi ya serikali ya CCM na ndo sababu mafanikio yake ni ya ndani ya nchi tu, tena kiubabe kama CCM yenyewe.
 
wa Tanzania ni wa midomoni,kama zilivyo siasa,labda waonge waamuzi kama wanavyopindua matokeo,lakini tukienda kimataifa zaidi hatuwezi,timu pekee inayojua mpira ni Azam lakini nao wanaonewa kila siku
 
Jana nimebahatika kuuona mchezo wa Yanga na Waarabu kupitia luninga. Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa kweli Yanga wanatakiwa wakaze buti vinginevyo wataambulia patupu. Jana wale Waarabu walitawala uwanja mzima na walikuwa wananacheza kama wanavyotaka. Pasi za Yanga hazikuwa maakini kabisa. Kwa siku hizi zilizobaki mfanye masahihisho makubwa. Lugha ya kuwa Waarabu hawachomoki ilikuwa ni danganya toto.
Mkuu,
Kwa mtazamo wangu umetumia lugha isiyo sawa na ya "kibaguzi"
Waarabu ndio team gani? Je kama wao wakiandika Al ahly wamecheza na "Waafrika" itakua sawa? Kwanini uandike "Waarabu" badala ya jina la team? Kuna nchi nyingi za kiarabu sasa hapo mtu atajuaje kuwa Yanga walicheza na team gani? Kumbuka JF inasomwa world wide,

Thanks.
 
Mkuu hongera kwa kusema ukweli kuwa Yanga ni taasisi ya serikali ya CCM na ndo sababu mafanikio yake ni ya ndani ya nchi tu, tena kiubabe kama CCM yenyewe.
kule pemba wanakoenda kujifua , nilihabarishwa ya kuwa wana -CUF woote ambao ni wapenzi wa yanga wameikimbia timu hiyo eti sababu sare zao ni za ccm,
 
Kuna watu humu huandika baada ya kupata viroba...
Yanga TIMU nzuri na hapa hatuongelei AZAM.
Makosa kidogo wenye timu tumeyaona ngoja turudi Cairo mtaisoma number
 
Mkuu hongera kwa kusema ukweli kuwa Yanga ni taasisi ya serikali ya CCM na ndo sababu mafanikio yake ni ya ndani ya nchi tu, tena kiubabe kama CCM yenyewe.

nawe acha kukurupuka ni wapi nimeyasema hayo, kaa ufikiri kwa makini
 
Back
Top Bottom