Mchezo wa Yanga naTownship Rollers Kumpaisha au Kumshusha Zahera

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Baada ya kufanyika usajili , jambo pekee ambalo mashabiki wa Yanga wanataka kuona, ni timu yao ikifanya vizuri

Ukiachana na michezo ya kirafiki ambayo Yanga imecheza, matokeo ya mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers hayakuwafurahisha wengi hasa ikizingatiwa mchezo huo ulipigwa ardhi ya nyumbani

Tayari baadhi ya mashabiki wameanza kuhoji uwezo wa kocha Zahera katika kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu

Ni jambo la kawaida hasa pale timu inapokuwa haipati matokeo ingawa bado ni mapema sana, lakini hali hiyo ilitarajiwa

Kwa misimu miwili Yanga haikuwa katika ubora wake wa miaka mingi, hivyo baada ya usajili wa nyota wengi wapya, mashabiki walitarajia kuiona Yanga mpya

Kocha Mwinyi Zahera anafahamu kama Yanga itaondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua hii ya awali, basi atakuwa kwenye wakati mgumu

Na pengine hiyo ndio sababu iliyomfanya achukizwe na ziara ya timu yake mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo alibainisha kuwa haikuisaidia timu kwa kuwa walicheza kwenye mazingira ya viwanja ambavyo haviendani na mazingira watakayocheza huko Botswana

Hata hivyo uongozi wa Yanga umesema ziara hiyo iliikuwa na manufaa na iliandaliwa kwa matakwa ya benchi la ufundi

Lakini jambo la msingi kwake ni kuhakikisha Yanga inashinda ugenini ili kuweza kusonga mbele raundi ya kwanza

Matokeo tofauti na ushindi, yatamuweka kwenye wakati mgumu mbele ya mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wameendelea kumuunga mkono licha ya kutoridhishwa na matokeo ya michezo ya hivi karibuni

Katika moja ya mahojiano yake, Zahera alisema wamedhamiria kushinda ugenini, lengo likiwa kupata bao mapema ili kuwaweka kwenye presha Township Rollers watakaokuwa wakicheza nyumbani

Pengine huu ndio mchezo ambao Wanayanga wataishuhudia ile timu yao halisi wanayoitaka

Lakini kama mambo yakienda 'kombo', mchezo huo utazidi kumpunguzia imani Zahera

Kwani siku zote, makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe pale inapotokea timu haifanyi vizuri.
 
mchezo wa mpira ushindi nipopote haijalishi upouwanja wa nyumbani ama ugenini na mwenyewe zahera katuamisha ushindi lazima sasa wacha tuone ila yanga ikitolewa kweli kazi anayo
 
Kwa msimu huu zahera hana pa kushika kama kweli timu itafanya vibaya,kwanza nadhani kwenye financials yanga ndo timu inayoongoza kwa kuwa na wadhamini kuliko timu yoyote inayoshiriki ligi kuu,kuhusu wachezaji wote waliosajiliwa ni pendekezo la mwalimu, mengine yatakayo tokea itakua ni ubovu wa mwalimu na hakuna kitu kingine..
Tatizo la zahera ni dharau,huyu bwana alikuja na fikra mbovu sana juu ya ligi yetu,yeye kuishi ufarasa alifikiri labda bongo hapa hakuna mtu amewai kufika ubeligiji,kwenye interview zake huwezi kumsikia akizungumzia maswala ya ufundi wa timu yake,mara zote yeye ni kukashfu viwanja,wqchezaji wa timu pinzani na viwanja..
 
Yanga ina wadhamini wangapi ambao ni wengi kuliko timu zote?acha ndoto mkuu nitajie wadhamini hao tuone.
 
Ndiyo Kwanza kapata kikosi kulingana na mahitaji yake. Itakuwa sio fair kumhukumu kwa sasa hata kama Yanga haitapita.
Kwenye first eleven, kutakuwa na Yondani, Boxer, Shishimbi na labda Feisal. Wengine wote watakuwa wageni. Lazima timu ipate muda wa kujenga chemistry kati yao.
 
Wanaohoji ni mashabiki maandazi wa mikia
 
Zahera ni kocha bora kabisa kwenye ligi kuu. Uwezo wa Zahera umeonekana msimu uliopita.Alito ushindani wa kutosha kwa timu iliyo sajili kwa bilion tatu nanusu wakati kikosi chake kilikua na thamani ya milion 200. Tena kikosi cha bilioni tatu kikiwa na viporo lukuki na marefa wakilazimisha matokeo.
 
Ongeza volume vyura wenzio wapokezane huku...
Mapinduzi cup alifanya nini?
Sportpesa cup alipata nini?
FA cup aliwapa nini?
Ligi kuu tu ndio ameonewa sio..? Mtateseka sana na huyo muuza dawa ya panya, mende, kunguni na viroboto.
Ongeza sauti"
 
Huyo ajiandae kucheza mayenu tu,mpira kama ilivyokuwa AFCON.
 
Hata mimi kwa utetezi huu niko na PaPaa.. Aachwe atengeneze timu aliyoitaka, sio kumpima kwa mechi 2 tu.
Ila kwa soka la Bongo lolote lawezekana
 
Hakuna kocha pale... Yanga ashatoka, kisichojulikana ni idadi ya magoal tu... Na baada ya game ya Yanga na Simba, Zahera ndo utakua mwisho wake na Yanga.... Note my words
 
wote tuuimbeeee ......Tuna imani na zaheraaaaaa tunaiman nayeeeeeeeee oyeeeeeee
 
zahera ni bonge la kocha huwez mlinganisha na uchebe .zahera angekuwa na timu kama simba mambo yangekuwa moto sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…