BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mchimbaji mdogo mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Eliya anaekadiriwa kuwa na miaka 28-30 amefariki dunia baada ya kuangukiwa na jiwe wakati akichimba madini katika machimbo yaliyopo eneo la Magema mtaa wa Nyamalembo mjini Geita.
Tukio hilo limetokea zikiwa zimepita siku mbili kufuatia tukio kama hilo lililotokea Kijiji cha Igando, Kata ya Magenge wilayani Geita na kusababisha vifo vya wachimbaji wanane baada ya shimo walilokuwa wakichimba kujaa maji kutokana na mvua iliyonyesha maeneo ya Milimani.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Geita, Hamis Dawa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea saa moja asubuhi wakati mchimbaji huyo akitoa udongo unaosadikiwa kuwa na dhahabu (fero) na jiwe kudondoka na kumponda.
Dawa amewataka wamiliki wa mashimo ya uchimbaji kufanya ukaguzi wa maeneo yao na kujiridhisha kama yapo salama ili kuzuia ajali zisizo za lazima na kusema jeshi hilo linaendelea na ukaguzi na mashimo yatakayobainika kuwa hatarini yatafungiwa.
“Tunaendelea na operesheni ili kuwashauri namna nzuri ya kukabiliana na ajali hizi tunawasihi mashimo ambayo sio imara wakati huu wa mvua yasitumike,” amesema.
“Aliyefariki alikuwa anafanya kazi chini shimoni wakati huo wenzake walikuwa juu wanapiga na ndipo jiwe kubwa lilichomoka na kumwangukia. Wakawa wanamsaidia kumchomoa, akavunjika mguu na mkono wakashindwa kumtoa, wakakapiga simu Zimamoto wakaja wakashirikiana na wachimbaji kumtoa akawa ameshafariki,” amesema Idd Haruna.
Mmoja wa wachimbaji wadogo anayefanya kazi eneo hilo, Regnald Sitta amesema chanzo cha kifo hicho ni ubovu wa shimo kwani lilishafungiwa lakini watu huingia kinyemela. Hivyo ameiomba serikali kufanya ukaguzi wa migodi ili ile mibovu ifungwe kisheria.
Amesema licha ya maeneo hayo kuwa na wakaguzi lakini rushwa ndio inasababisha matukio kama haya kutokana na wao kuruhusu wachimbaji wanaoingia kinyemela maarufu ‘manyani” kuingia kwenye shimo kwa wizi licha ya wao kujua shimo ni bovu.
MWANANCHI