Mfanyabiashara na Mchimbaji mdogo wa Madini na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kuruthum Issa Runje, amechangia kiasi cha Shilingi milioni 4,555,183 kwa ajili ya kukata Bima ya gari chama hicho Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Runje alimkabidhi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Nachingwea Emmanuel Mbamage risiti ya malipo yenye thamani ya kiasi cha Sh. Milioni 4,555,183 kwa ajili ya Bima ya gari ya CCM ili gari ili liendelee na kazi za Chama.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Nachingwea Emmanuel Mbamage ametoa shukrani za dhati kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi kwa kwa kukisaidia Chama cha Mapinduzi hasa kwa kupindi hiki kuelekea katika shughuli za uchaguzi.