Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mchina Anayedaiwa Kuanzisha Mgodi wa Madini ya Ulanga Kinyemela Kusakwa
Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa amemwagiza afisa Madini mkoa wa Songwe kushirikiana na Ofisi ya Halmashauri ya Momba kumsaka popote raia wa kichina ambaye jina lake halijafahamika kwa kosa la kuanzisha mgodi wa kuchakata madini ya ulanga kinyemela eneo la Kijiji cha Ntungwa kata ya Mkomba ndani ya Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri Kiruswa amefikia uamzi huo baada ya kupokea taarifa akiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Itumbuka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Momba Mheshimiwa Condester Sichalwe (Mundy) juu ya uwepo wa taarifa za mtu huyo kuanzisha kiwanda bubu cha kuchimba na kuchakata madini hayo.
Baa ya kupata taarifa hizo, ndipo Naibu Waziri akafunga safari mpaka eneo kilipo kiwanda hicho, na kukuta uzalishaji ukiendelea, tayari mzigo ukiwa umefungwa kwenye viroba vyenye uzito wa tani 50 tayari kwa kuusafirisha.
Hata hivyo Naibu Waziri baada ya kufika eneo la tukio hakuweza kumkuta mtu yeyete ispokuwa mzigo na mashine mbili za kuchakatia madini hayo, na ndipo akaagiza afisa Madini mkoa wa Songwe Chone Malembo kumtafuta mtu huyo na kumhoji ni kwanini anafanya kazi hiyo bila leseni.
Aidha uongozi wa Halmashauri kupitia Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Ntungwa amesema hata wao hawana taarifa za mtu huyo, ispokuwa siku za hivi karibuni mtu huo ambaye ni mchina alionekana kujenga kempu site na kuendelea na kazi ya uchakataji