Uchaguzi 2020 Mchinga: Polisi watumia Mabomu ya Machozi kuvuruga Mkutano wa ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Mchinga: Polisi watumia Mabomu ya Machozi kuvuruga Mkutano wa ACT Wazalendo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Polisi watumia Mabomu ya Machozi kuvuruga Mkutano wa @ACTwazalendo ulokuwa ukifanyika katika Kiwanja cha Legeza Mwendo Kata ya Milola Jimbo la Mchinga.

Mgombea wetu, Ndugu Syprian Mtotomwema, Mkutano wake umevurugwa ili kumpisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kumnadi Salma Kikwete. Pamoja na kwamba Mkutano wa Majaliwa ulikuwa ukifanyika Milola Centre; Kilometa kama 5 kutoka ulipokuwa ukifanyika mkutano wetu, lakini bado Polisi walitutaka tuvunje mkutano wetu; jambo ambalo hatukuwa tayari kulikubali.

Tuna ratiba ya kufanya mkutano kiwanja cha Legeza Mwendo na zaidi kwa umbali uliopo baina ya maeneo hayo, hakukuwa na sababu ya msingi ya mkutano wetu kusitishwa. Hizi ni hujuma za dhahiri kabisa! Na kwa hakika zinautia doa uchaguzi wa mwaka huu.

#ZIKOMESHWE!
 
Jimbo la Mchinga hilo!!

Nilishawahi kusema hapa kwamba Mama Salma kashauriwa vibaya sana kwenda kugombea Mchinga manake pale hawezi kushinda kwa haki hata kama wanaweza kumtangaza kwa kuficha aibu ya ex0-First Lady kushindwa!!!
 
Back
Top Bottom