PostGE2025 Mchinjita: Hakuna matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2025 kwenye Gazeti la Serikali

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo bara, Isihaka Mchinjita, amehoji ukimya wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kushindwa kuchapisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwenye Gazeti la Serikali, akidai kuwa muda wa kisheria wa kufanya hivyo umeshafika ukomo.

1768369314962.jpeg

Akizungumza jana, Januari 12, 2026, katika mkutano wa ndani na viongozi pamoja na wajumbe wa Jimbo la Segerea mkoani Dar es Salaam, Mchinjita amesema kuwa kushindwa huko kwa Tume kuweka matokeo hayo hadharani, ikiwemo kwenye tovuti yao rasmi, ni ishara ya "wakati mgumu" na mashaka juu ya uhalali wa tarakimu zilizomtangaza mshindi.

Aidha Mchinjita ametoa wito kwa Watanzania kusimama imara kulinda thamani ya uraia wao, akionya kuwa vitendo vya ukatili, utekaji, na hujuma za uchaguzi havitaisha ikiwa wananchi watabaki kuwa watazamaji.

Pamoja na unafiki wa viongozi wa ACT
Ila hapo wamesema ukweli
 
Hawa mbuzi tu, wangegomea kitambo uchaguzi usingekuwepo, wanasiasa ndumi la kuwili
 
Kwenye kutangaza yale matokeo na asilimia zake za mchongo; lilikuwa ni zoezi jepesi sana! Shughuli ipo kwenye kuoanisha hizo taarifa sasa!!

Yaani ni rahisi sana kufanya makosa na kuonekana hadharani hiyo INEC nani sijui imepika taarifa zake.
 
Back
Top Bottom