Pre GE2025 Mchinjita: Watu wanaambiwa wanunue maiti za ndugu zao, serikali ilitangaza ajira za walimu 8,000 2024/2025 lakini kilitoka kibali cha nafasi 4,000

Pre GE2025 Mchinjita: Watu wanaambiwa wanunue maiti za ndugu zao, serikali ilitangaza ajira za walimu 8,000 2024/2025 lakini kilitoka kibali cha nafasi 4,000

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Source #1
View Source #1
Mchinjita alikuwa na mkutano wa hadhara mkoani Mtwara ambapo amezungumzia masuala mbalimbali, tazama hapa hotuba yote.

mchinjita.jpg
 
Tunachokijua
Isihaka Mchinjita ni makamu mwenyekiti Bara wa Chama cha Act-Wazalendo ambaye alichaguliwa na mkutano mkuu wa chama hicho kwa kupata kura 517 sawa na asalimia 96.5, machi 6, 2024. Mchinjita alifanya mkutano wa hadhara mkoani Mtwara terehe 5/12/2024 ambapo akiwa huko alizunguzmia mambo mbalimbali na kutoa baadhi ya madai ambayo baada ya uhakiki yamebainika ni ya kupotosha.

Madai ya watu kuuziwa maiti za ndugu zao wanapofariki wakati wakipatiwa matibabu katika vituo vya afya

Machinjiti alidai kuwa wananchi wanaambiwa wanunue maiti za ndugu zao mara wanapofariki wakiwa wanapatiwa matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wapate nafasi ya kupewa miili hiyo wakaizike.

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa yanapotosha kwani hakuna watu wanaoambiwa wanunue maiti mara baada ya ndugu zao kufariki, na badala yake huwa wanatakiwa kulipa gharama za matibabu ili waweze kupewa maiti yao.

Kwa kulitambua hilo wizara ya afya ilitoa waraka namba moja wa mwaka 2021 wa kutokuzuia maiti na kuweka utaratibu wa kulipia gharama za matibabu na madeni kwa miili. Ambapo katika waraka huo uliohifadhiwa hapa umeeleza kuwa kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu changamoto wanazokutana nazo wakati wa kuchukua maiti za ndugu zao kutoka kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti wameamua kuandaa waraka wenye muongozo wa namna ya malipo na kuchukuliwa kwa miili bila usumbufu.

AD_4nXePXOvDeQM0zMgqAFDTcTw9jHAI8ysuLcFZdE3XYlHZmd3jK6Dxsa9EaCqNgSIOlrPWavnusb3zZ78Sw9yM3JlQBxarPXjOkGhxWh5kWN96zH7f1uaP2A5wLytlWdgB5Ssoxm3F


Hivyo suala la kununua maiti ni la kupotosha na badala yake ki uhalisia kinachotokea ni kuzuiliwa kwa miili ya marehemu kutokana na madeni yaliyotokana na matibabu wakati wa uhai wa marehemu.

Uhalisia wa madai kuwa zilitangazwa nafasi za ajira 8,000 za walimu lakini Rais Samia alitoa kibali cha kuajiri walimu 4,000. rejea video hii dakika ya 33.

Madai ya Mchinjita kuwa serikali ilitangaza nafasi za ajira 8,000 kwa walimu si ya kweli na ni ya kupotosha kwani idadi hiyo ya nafasi za ajira za ualimu mwaka 2024 kuelekea 2025 haikuwahi kutangazwa.

Julai 20, 2024 serikali ilitangaza nafasi 11,015 za ajira kada ya ualimu ambapo awali Mei 9, 2024 Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Zainab Katimba alisema mwaka wa fedha 2024/25 walimu 12,000 wataajiriwa na watapangiwa vituo vya kazi katika maeneo yenye upungufu.

Mnamo tarehe 23, Novemba, 2024 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akifungua Mafunzo elekezi kwa maafisa Uthibiti ubora wa shule wa wilaya yaliyofanyika jijini Dodoma alisema serikali imetoa kibali cha kuajiri walimu 4,000 wa somo la biashara kwa ajili ya kufundisha wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, wakilenga kuwapa maarifa muhimu kupitia mtaala mpya wa elimu.​
Back
Top Bottom