japanese
Member
- Jul 28, 2015
- 13
- 16
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na hii dhana ya uchochezi hasa kupitia mitandao ya kijamii. Dhana hii sasa imekuwa ni kibano kikali kwa watoa maoni wote katika mitandao na wengi wetu tumeathiriwa kwa namna moja au nyingine. Wengi wa wanaoingia kwenye kadhia hii huishia kuwa na mashtaka ambayo yanakosa mashiko kwenye vyombo vya haki kwa kukosekana kwa ushahidi uliobayana kuwatia hatiani.