Mchongo wa Biashara ya magari ya maji taka hapa Dar

Mchongo wa Biashara ya magari ya maji taka hapa Dar

Tella Mande

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Posts
494
Reaction score
675
Mimi ni transporter wa muda mrefu toka coaster kuja fuso mpaka sasa malori. Ninaona kama fursa ipo kwenye biashara ya malori ya maji machafu haswa haya makubwa ( lita 15,000 hadi 20,000)

Natamani kupata uzoefu wa walioko kwenye hii biashara....

1. Njia nzuri na rahisi ya kupata haya malori. Ikiwezekana mitandao yake.
2. Gharama za kusajili nk
3. Biashara inavyofanyika. Naona madalali wamefunika madereva kabisa.
4. Hesabu kwa tajiri imekaaaje...nk

Naomba wenye kujua waniweke wazi hapa.
 
Hili jukwaa lina watu wengi sana wenye ujuzi na werevu wa mambo kibao endelea kusubiri watakuja kukupa muongozo
 
Back
Top Bottom