TANZIA Mchora katuni gazeti la Mwananchi, King Kinya afariki dunia

Pumzika kwa amani King Kinya. Ulipokuwa unawachora watawala nilijua tu wasiojulikana lazima wangefanya mambo yao. Nchi hii ukiwa mkosoaji wa serikali maisha yako yatakuwa mafupi sana. Ngoja tu tuenddelee kuwa machawa. Bado tunapenda kuishi.
 
Hata kama angepelekwa huko unakokutaka wewe,kama siku imefika,haicheleweshi hata sekunde moja
Hakuna aliyekataa siku yake ilifika elewa hoja ya msingi ni kwenda kupambania afya mkoani ambako hakuna huduma bora za afya kama Dar alikoanzia kuugua.
 
Sahihi kabisa, Kuna mtu namfahamu Ni jamii ya masai aliugua mda mrefu akawa analala tu akipatiwa matibabu MNH mwisho wa siku wakampeleka kutibiwa kienyeji umasaini hali ilivyozidi kuwa mbaya wenyewe wakamrudisha tena MNH lkn baadae akafariki, tabia za kuingiza imani za kurogwa huwa zinatokea kwa ndugu pale wanapoona ndugu yao haponi na matibabu anapata.

R. I. P King.
 
Pumzika kwa Amani ndugu. Vibonzo vyako havikuwa na kelele, ni picha tu tunaelewa na kufurahi. Pengine ungekuwa nchi za wenzetu ungekuwa billionea na kuiacha familia yako na wanao na uzao wako wakineemeka na uwezo/akili yako, Ila Africa hii sidhani.

Sala zangu na maombi yako yawe juu yako. Amina.
 
Jina lake halisi ndiyo hilohilo la King Kinya?
Mbona wamamtangaza kwa jina maarufu pekee?
 
ukute miccm ndio imemuua
 
Una insight nzuri lakini inaenda kinyume na logic.

Mfano kijijini kwenu kuna mgonjwa wa kansa hospitali ya wilaya ya kijiji chenu ikampa rufaa aende Mhimbili kwa matibabu zaidi.

Mhimbili wakahandle sehemu yao kisha wakamuambia mgonjwa kwa palipobaki inabidi aanze tiba ya mionzi Ocean Road.

Huyu mgonjwa anasema mionzi itamuua bora akale mitishamba. Anarudi kijijini kwenu. Kisha anazidiwa, mnamrudisha tena hospitali ya wilaya, ambayo mwanzo kabisa iliona haina uwezo ikatoa rufaa.

Mgonjwa anafariki. Mfano wa hii sequence ya matukio inaweza kukupa picha kwanini kumuondoa marehemu Dar haikua jibu sahihi.

Wanaotibiwa Dar wanakufa, lakini wanakua karibu na kila fursa ya kupona kuliko aliyepo Kakonko kwa ugonjwa ule ule. Kituo cha Afya cha Magomeni Dar kinahudumia wagonjwa wengi kuliko hospitali za wilaya za mikoani.
 
Una insight nzuri lakini inaenda kinyume na logic.

Mfano kijijini kwenu kuna mgonjwa wa kansa hospitali ya wilaya ya kijiji chenu ikampa rufaa aende Mhimbili kwa matibabu zaidi.
Umetoka nje ya uhalisia na kuchagua kutoa mfano ambao utasupport ulicho kisema,hapa wala hatujaongelea issue ya Wilaya wala Kijiji,tumeongelea Hospitali nje ya Dar,ndio maana nimekwambia kua umetoa mifano ambayo utaona ina support ulichokisema,
Mhimbili wakahandle sehemu yao kisha wakamuambia mgonjwa kwa palipobaki inabidi aanze tiba ya mionzi Ocean Road.

Huyu mgonjwa anasema mionzi itamuua bora akale mitishamba.
Kama kaamua kula miti shamba na kukataa matibabu ya hospitali,hiyo ndio justification ya kuona kua Hospitali nje ya Dar hazina matibabu bora? umechagua kutoa mfano wa Cancer coz unajua Hosp kuu ipo Dar,mgonjwa kukataa matibabu na kwenda kwa waganga wa kienyeji ndio ina maanisha kua,Hospitals bora zipo Dar peke yake? issue ya kwenda kwa mganga wa kienyeji inahusiana vipi na ubora wa matibabu ya Hospitali?
Anarudi kijijini kwenu. Kisha anazidiwa, mnamrudisha tena hospitali ya wilaya, ambayo mwanzo kabisa iliona haina uwezo ikatoa rufaa.
Sasa hapa hili ni tatizo la mgonjwa kukataa matibabu au Hospitali kutokua na matibabu bora?
Naona umetoka kabisa kwenye mada,hii mifano yako wala haihusiani na nilichokisema kuhusu ubora wa matibabu ya Hospitali.
Mgonjwa anafariki. Mfano wa hii sequence ya matukio inaweza kukupa picha kwanini kumuondoa marehemu Dar haikua jibu sahihi.
Ndio maana nikakwambia kua,mgonjwa anaweza kufia popote pale,hata wanao enda India na Europe hufia huko pia,
Wanaotibiwa Dar wanakufa, lakini wanakua karibu na kila fursa ya kupona kuliko aliyepo Kakonko kwa ugonjwa ule ule.
Una data zozote za kusupport ulichokisema hapa?
Kituo cha Afya cha Magomeni Dar kinahudumia wagonjwa wengi kuliko hospitali za wilaya za mikoani.
Sasa kuhudumia wagonjwa wengi inahusiana nini na ubora wa matibabu? hujui kua Dar ina population kubwa? so,hata wagonjwa ni lazima watakua wengi?
 
Cases za namna hiyo ni nyingi mno.

Nilizishuhudia zaidi kanda ya ziwa, hasa usukumani. Katika jamii ya wasukuma kwa % kubwa mtu hadi apelekwe hospitali hali inakuwa ni mbaya haswa! Kichwa kikiuma kidogo tu kwa mganga kwa mambo mawili:
1. Kutibiwa
2. Kupiga ramli ili kujua ni nani kafanya mchezo mchafu ili kisasi kifanyike

Angalau kadri muda unavyoenda nao wanapunguza. Ila nina wadau wa kutosha tu ambao ni wasomi kabisa lakini wakiugua au kuuguza bado wanaanzia kwa waganga.

Mmoja ana dada yake mwenye dalili za saratani ya ubongo, lakini walishaweka kambi ya kudumu kwa 'mtaalam' na ushauri wa kwenda kupima hospitali hawapokei kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…