Mchora katuni Mtanzania, Mohammed Jumanne (Meddy) ashinda Ufaransa

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Mchoro wa katuni ulioandaliwa na msanii ndugu Mohammed Jumanne almaarufu Meddy kutoka Tanzania imechaguliwa kuwa Nembo ya Ushirikiano mpya kati ya Afrika na Ufaransa (New Africa-France Summit) uliofanyika jana Oktoba 08, 2021 nchini Ufaransa

Meddy ni mchoraji katuni wa kujitegemea hapa nchini.




Pichani:

Siku ya juzi tar 8 Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisalimiana na mchora katuni Meddy kutoka Tanzania, siku hiyo hiyo mchora katuni Optatus Fwema alishtakiwa katika mahakama ya kinondoni jijini Dar es salaam kwa kumchora Rais Samia Suluhu. What a contrast!

 
Hongera zake ,watu wakitoka nje ya Tanzania wanashinda.Najiuliza maswqli mengi sana ni kuwa sera zetu hazimwandai mtu kuwa exposed na hivyo vitu au siasa hazitaki mtu aonekane au tuko busy na matatizo yetu bila kuangalia kidogo tunachokiwezo anyway Hongera zake
 
BASATA ipo kwenye kudhibiti na kufifisha vipaji.

Hii fursa huyu kijana ameipigania nje ya mfumo wa wizara. Kuna fursa zinakuja nyingi lakini maafisa wa wizara na BASATA wanawaunganisha jamaa zao hivyo huko nje sanaa yetu inaonekana changa mno.

Mfumo uliooza hauwezi kuzalisha tija
 
Team ya Olympic inakuwa na maofisa wengi wa serikali kuliko wanamichezo. Huu ni mfano mmoja tu, hela za maandalizi pia zinatoka kwamanati.
 
Wale ndugu zetu hawajajua Kama anatokea kwao wajipongeze.
Ni Mtanzania
Najua kuna wapuuzi watajitokeza kusema ushindi huu ni sera yao nzuri.

Juzi hapa wamemtoa kamasi mwenzetu kwa kumlaza ndani bila kosa kwa wiki mbili
 
Hongera sana kwa kutuwakilisha vema. Natumai sasa Optatus Fwema nae ataapata jukwaa la kutambulika
 
Umefanya heshima kubwa kumjibu huyo zuzu
 
"Keep it Simple but Impactful"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…