Mchumba wa aunt ezekiel afunguka: "wanawake ni wauaji"......ni baada ya kugundua kuwa aunt kafunga n

Mchumba wa aunt ezekiel afunguka: "wanawake ni wauaji"......ni baada ya kugundua kuwa aunt kafunga n

Gumzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Posts
211
Reaction score
8
SIKU chache baada ya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kuripotiwa kufunga ndoa mjini Dubai, mchumba wa staa huyo aliyetambulika kwa jina moja tu la Jeff amesema kuwa, anashangazwa na Aunt kuolewa huku akiwa na ujauzito wake.

Akizungumza jijini Dar hivi karibuni, Jeff amesema kuwa taarifa za kuolewa kwa Aunt alizipata akiwa nchini China na kushtuka sana.

"Kinachonishangza ni huyo jamaa anafungaje ndoa na mwanamke ambaye ana ujauzito wangu wa miezi sita ambao aliondoka nao kwenda Dubai?" alihoji Jeff.

Jeff aliendelea kutiririka kama mtu alikuwa akiimba mashairi ya Muziki wa Injili kuwa, kingine kinachomuumiza ni tabia ya Aunt kumuomba fedha za matumizi akiwa Dubai huku akijua kwamba amefunga ndoa na mtu mwingine.

"Wanawake ni mama zetu lakini ni wauaji wakubwa, inakuwaje anagawa mimba ya mtu kwa mwanaume mwingine halafu mbaya zaidi nilipokuwa China kila wiki alikuwa akiniomba fedha za matumizi nami nikawa namuagiza aende sehemu kuchukua kumbe ni mke wa mtu!" alishangaa Jeff.
Juhudi za kumpata Aunt ili kuthibitisha madai hayo ya ujauzito hazikuweza kufua dafu baada ya simu yake anayoitumia huko Umangani kutokuwa hewani. KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA http://moses-ayoub.blogspot.com/2012/07/mchumba-wa-aunt-ezekiel-afunguka.html​
 
Mimba anajua mwenyewe Aunt ni ya nani. Huyo kaka anajicholesha tu angekaa kimya.
 
Kuhusu kuomba ela... anachuna za mwisho mwisho. Lol. Mjini shule.
 
Uhuni mwingine wa kitoto sana. Shoga na mimba wapi na wapi wananangu kama siyo kuchanganyikiwa au kutafuta sifa rahisi?
 
watayamaliza wenyewe, sisi yetu macho na masikio.
 
Kwani hata kama ana mimba yake ndio akae aishi mwenyewe na mtoto. Inaelekea kuwa hawapo wote na anataka Ezekiel asiwe na bwana mwingine sababu ya mimba yake, kweli anachekesha huyo anayedai ni baba mtoto.

Afanye DNA akizaliwa baby. Na kama yeye baba atakoma lazima alipe matumizi analo.
 
Wajinga ndo waliwao! Huyo Jeff ana uhakika gani kua mimba ni ya kwake?
 
Huyo jamaa ni taahira kabisa, badala ya kushukuru mungu kumuepushia kikombe hicho analalamika!!! Hivi alikuwa anataka kufuga kunguru?! amshukuru mungu kwa kupoteza hivyo visenti na hiyo "mimba' (kama ipo kweli) kuliko mateso ambayo angepata kwa kumuoa
 
Huyo Jeff amesahau kwamba anayemjua Baba wa mtoto ni Mama na si mwingine....
 
Back
Top Bottom