Mchumba wangu ni mzuri sana

Jiamini kaka, wazuri wengi wapo wametulia kwenye ndoa zao, inaonekama unashindwa kujiamini wewe
 
umesema anakupenda...sidhani kama kuna tatizo hapo mkuu...ungeniambia hajaseto hapo ingekuwa ishu.halafu jua kwamba uzuri wa kitu upo machoni mwa mtazamaji...
asante. Ngoja nikaze buti.
 

Jiamini u r the only one to her
Wala usipoteze au kujipa presha bure kuwa kuna watu wanamtanani
Wewe kama anakupenda ni wewe onyesha upendo wa dhati kwake na amini u r the only man to her
Hayo mengini ni presha tupu
 

....sasa kinachokuumiza ni huo uzuri wake au huko kutongozwa?
 
uzuri wa mtu uko machoni mwa mtu, kama vp mmwage tafta sura mbaya upunguze presha
 

Mkuu ..naogopa kukushauri..lakini Anyway..I will give it a shot..

Mimi binafsi naona unakosea sana kujenga akili yako kama unampenda mpenzi wako kwa sababu ya uzuri wa sura.. May be I am wrong..lakini... kama utaendelea kujenga hiyo dhana na akili yako.. ni rahisi hiyo akili yako hapo baadaye kukusaliti kwani ipo siku itakupa comparison na mwingine na kutoa maksi nyingi kwa huyo mwingine wa mtaani..ukiingia kwenye huo mtego umekwisha..

Kumbuka sura, maumbile na miili yetu inabadilika kwa muda mfupi.. maisha ya ndoa yana kupanda na kushuka....sasa ndugu yangu ukipenda sura ..halafu ukafika siku ile ambayo maisha yameshuka kwa ka-bump ndogo..hutakawia kuona changudoa ni mzuri..Ushauri wangu.. mpende huyo binti kwa vyote..tafuta na invent chochote..sauti, figure, akili, yaani changanya vyote..ili hapo baadaye kimoja kikipungua na ..kingine kinafidia..gap..
 
Sasa siutafute mbaya ukae kwa amani kama huyo hakupi amani? Mwanaume halafu unakuwa hujiamini
 

Kwanza we una umri gani????? maana unayoyaandika inaonyesha aidha umri umeenda zaidi au ni mtoto kabisa?
 
Kila mtu ni mzuri kwa mpenzi wake.
Bibi kidude pia mzuri kwa mmewe.
 

mwambie amuache...
 
Mbona mnamjibu Tigga Mumba kama mwanaume?
Mi TM naemjua ni mdada jasiri mno aliishi kama MKIMBIZI na kama cjakosea aliolewa na John Vata! Anyway... Labda ni majina tu yamefanana!
 
Jamani ila kuna wanawake/wanaume ni wazuri hata kama kuna usemi uzuri ni subjective. Kuna watu kila mtu anakubali kuwa wana mvuto unakuta ni msichana akipita hata wasichana wenzie lazima wageuke. Wapo watu wa hivyo ila ni wachache kwa hiyo mtoa mada ana haki ya kusema wife to be ni mzuri.

Ushauri wangu ni kuwa kama tabia yake ni nzuri kama yeye mwenyewe usitie shaka; ila kama ni mapepe jua hata ukimtia hiyo mimba akishazaa ataendelea kugawa. Maana in most cases hao wanawake/wanaume wazuri kupitiliza utulivu unakuwa zerooo. Ila kama umebahatika kukutana na mtulivu usitie shaka.

Nina uncle wangu alioa mke mwenye uzuri wa hajabu yani alikuwa ni gumzo la mtaa. Afu ana roho nzuri ambayo sijawahi kuona. But alikuja kufa kwenye MV bukoba kila mtu aliamini usemi kuwa vizuri havidumu (but am not saying kuwa wazuri watakufa ila nasema kuna wazuri ambao na tabia zao ni nzuri pia).
 

Take it easy as long as she is yours, na umesema mwenyewe anakupenda sana! Maelezo yako yanaonyesha uko INSECURE...Yaani unaona kama vile you don't deserve her kitu ambacho ni kibaya sana endapo atagundua. Anaweza kukunyanyasa sana kisaikolojia. Jiamini na mambo yatakuwa sawa tu!
 
Tigga Mumba unaposema mpenzi wako ni mzuri unamlinganisha na nani ? inawezekana kabisa mimi nikamwona mbaya,kuna dada wanamwita Fideline ye anadai ni mwana mitindo mi namwona mbaya sana lakini kuna watu mjini wanakwambia hamna mzuri kama yeye,nadhani hapo umenielewa.
 

.....Ila mkuu kuna wanawake ambao wako generally accepted kwamba ni wazuri, mfano wa akina Kim Kardashian au yule mtawala wa Misri - Cleopatra. Ukisimama kukana kwamba si mzuri watu wanaweza kukushangaa mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…