Mchungaji anafundisha Bible Knowledge na dini shule ya serikali.Je,halali?

Status
Not open for further replies.

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
413
Reaction score
90
Songea kuna mchungaji anafundisha Mashujaa sekondari.Amepangwa maalumu kwa kazi hii tu shule ya 'serikali'.Ni halali?
 
Sijui unataka kumaanisha nini au kuna la zaidi. Si anafundisha wakati wa kipindi cha dini au?
 
ulitaka kipindi cha bible knowledge afundishe sheikh acha ujinga. Kama walimu hawaijui bible knowledge nani wa kuwafundisha watoto?
 
Viongozi wa dini huwa wanaruhusiwa kwenye vipindi vya dini. Au haujasoma shule za Tanzania? Tena tangu shule za msingi.
 
Mimi naoona halali kabisa. Nilipokua O'level (shule ya umma) tulikua na kipindi cha dini na tulikua na mchungaji na waislam walikua na Sheikh/imamu! Waliosoma bible Knowledge walikua na Mchungaji wao, Islamic Knowledge walikua na Sheikh pia. Kila mtu alifundishwa kwa imani yake!
Naamin aliyeweka huu uzi alisoma shule zisizo na utaratibu huo!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwani ck hizi mashuleni hakuna vipindi vya dini, wkt wa kipindi cha dini, waislam wanaenda kwenye islamic knowledge vivyo hivyo kwa wakristo au wewe ni mgeni hapa tanzania
Songea kuna mchungaji
anafundisha Mashujaa sekondari.Amepangwa maalumu kwa kazi hii tu shule
ya 'serikali'.Ni halali?
 
Ninavyojua hilo ni jambo la kufurahi na kushukuru.Mbona B/knowledge na Islamic vinasaidia sana ufaulu?Viko ktk ratiba!!
 
Huyu mleta mada kwa jinsi alivyokurupuka ni wa kuhurumia.
 
Wadahu,kinachoshangaza ni kuwa ana vpnd vya darasani km wlm wengine.Pia anawaambia wakazane B/knowledge itawainua.Kivip?
 
Ruksa mkuu kwa anae taka hata masheikh na makekista huwa wanakuwa na vipindi kwa juma mara moja kinaitwa kipindi cha dini
 
Jamani Songea wabishi lol!Kwani huyu hajui kuwa mtu akiwa D na C na A ya Islamic au B\knowledge tayari imemuinua?Lol!
 
Bible Knowledge kama ilivyo Islamic Knowledge ni masomo yanayofanyiwa mtihani wa taifa! Kwa nini sasa msifundishwe ama wasifundishwe wale wanaohitaji?!

Uko kidato cha ngapi?! Yaani kufundishwa bible pia inaonekana kuwa nongwa?!

Ungekuja na uzi kuwa labda mnalazimishwa kusoma somo hilo ningeelewa, vinginevyo unaleta upuuzi na utoto tu usio na msingi humu!
 
Msameheni mleta mada naye kajaza server.
 
Mleta thread hii yawezekana hajasoma shule zetu za Tanzania, yawezekana ni moja ya matunda ya shule za Uganda.Hilo lipo wazi tena kuanzia Shule za msingi, somo la dini lipo.
 
Mimi ni mwl shule ya serikali katika vipindi vyetu vya shule masomo ya dini(islamic na bible knowledge) tumevipangia muda kama hesabu au somo lingine.
Pamoja na kuwa nafundisha math's pia nafundisha islamic kama ratiba ya shule ilivyopangwa na wenzetu wanafundishwa na mchungaji hakuna tatizo.
Tatizo ni kwamba baadhi ya shule wanaweza wakawa wanasoma bible knowlegde ila islamic hawasomi kwakukosa mwl. So waislamu wanaweza hisi wanadhulumiwa na yawezekana mleta maada pia ana mawazo hayo.
 
Wadahu,kinachoshangaza ni kuwa ana vpnd vya darasani km wlm wengine.Pia anawaambia wakazane B/knowledge itawainua.Kivip?

Bible Knowledge na Islamic knowledge ni masomo kama yalivyo masomo mengine! Yanawasaidia watu katika ufaulu wa mitihani ya form 4 kwan hua yanajumuishwa katika alama za ufaulu (angalia shule za seminari). So ni sawa kuwaambia wanafunzi wakazane.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…