Mchungaji auliwa na muumini aliyepandwa na mapepo

Mchungaji auliwa na muumini aliyepandwa na mapepo

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Mchungaji wa Kanisa la Agule Pentecostal Assemblies of God (PAG), Wilaya ya Serere, Uganda, John Michael Ekamu (52) amefariki Dunia baada ya kushambuliwa na muumini anayedaiwa kuwa na mapepo wakati wa lbada ya mkesha wa Krismasi

Wakati wa maombi ya mkesha huo, muumini huyo, anayejulikana kwa jina Osagani, alimpiga teke Mchungaji Ekamu, ambaye alianguka. Hata hivyo, alijitahidi kuendelea na ibada hadi alfajiri ya Krismasi.

Asubuhi ya siku hiyo, hali ya Mchungaji Ekamu ilibadilika ghafla, na alianguka tena madhabahuni. Waumini walipendekeza apelekwe kituo cha afya kwa matibabu, lakini alikataa, akiamini kuwa 'shetani ameshindwa."

Hata hivyo hali ya mchungaji huyo ilipoendelea kuwa mbaya alikubali kupelekwa kituo cha afya, ambako alifariki Dunia wakati wa upasuaji.

Muumini huyo aliyempiga teke Mchungaji ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 30 amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.

Copy and paste from Maulid Kitenge
 
Mambo mawili ya kujifunza:

1. Kuna watu wana matatizo ya akili (ukichaa) sio kila kitu ni mapepo. Utashangaa muuaji akienda kupimwa anakua declared kichaa na hakuna kesi

2. Maisha haya usimguse mtu. Kuna watu wanatembea na magonjwa ukimpiga hata kofi tu unaweza shangaa anajinyoosha unaishia kwenda kunyea ndoo.
 
Back
Top Bottom