Mchungaji auwa

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa hawezi kuongea na alikuwa amewekewa oxygen.



Siku moja Mchungaji akaenda kumuombea. Akiwa katika maombezi, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi akaandika halafu akampa yule mchungaji, ghafla mgonjwa akakata roho. Mchungaji hakukisoma kile kikaratasi wakati ule akijua ni wosia wa marehemu,



Akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema "Kuna kitu nilipewa na marehemu siku niliyokuwa namuombea". Akampa ndugu mmoja asome, kiliandikwa



'UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA
 
We Mwiba utakuwa mtambo ..kwenye Jokes na Utani hakuna Breaking Newz, halafu hii kitu kuna mdau alishaileta hapa kitambo..msitujazie jamvi kwa vitu visivyoeleweka ..ebo!
 
kwa kuwa inmhusu mchungaji? si joke tu? siku iliyoletwa hapa baadhi ya memba hawajaiyona, wacha wajikumbushe bwana we!
 
kwa kuwa inmhusu mchungaji? si joke tu? siku iliyoletwa hapa baadhi ya memba hawajaiyona, wacha wajikumbushe bwana we!

Wewe utakuwa una matatizo yaleyale yanayomkabili huyu mkalia-mwiba..lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…