Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mchungaji kutokea Kanisa la Pentekote, Davina Kahwa ameibuka hivi karibuni kuzungumzia uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika 2025.
Mchungaji huyo ambaye pia anatokea kwenye huduma ya uombaji wa kitaifa na kimataifa amedokeza kuwa uchaguzi huo unaokuja hautakuwa wa kawaida na kwamba
Uchaguzi wa mwaka 2025 utakuwa ni uchaguzi ambao haujawahi kutokea Tanzania. Sasa mtanzania, mtumishi wa Mungu tunahitaji kuwa na umoja. Watumishi wa Mungu wazee wetu ambao mmetutangulia hawa waumini tunawapeleka wapi?
Mchungaji huyo pia aliendelea kuhusu ukimya wa viongozi wa dini kwenye matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini
Kama mauaji yanaendelea hata kama atakuwa amekufa mtu mmoja maana ni kwamba atakuwa amekufa sio kwa mapenzi ya Mungu. Kwanini huyu mtu afe? Lakini sasa hivi tunaogopa hata kutembea. Nikwambie mtanzania, nikwambie mwana wa Mungu majira haya sio ya kukaa kawaida.
Source: Jambo TV