Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Ngosha Paskali,
Sio rahisi sana mtu kukuelewa unachomaanisha,nimekuwa nikikufuatilia uandishi wako siku hizi,inahitaji umakini kukuelewa unamaanisha kitu gani.
Ingawa tu ushauri wangu kwako, ni kuachana na hawa wapakwa mafuta wa Bwana....wao wajua ni Mungu yupi wanamtumikia,wewe kama muumini yakupasa uangalie ni wapi unapata chakula kikushibishacho kiroho. Kurumbana nao,wewe waache wao na Mungu wao,maana najua humu ndani ya JF kuna waumini na kanisa la Ufufuo na Uzima na unachoandika kinaweza kuleta mtafaruku wa ajabu sana. Huwezi kujua,huyo huyo mchungaji ambaye wewe huna imani nae,kuna watu waliopata uponyaji kupitia yeye! Sasa unataka kuwaambia nini watu hao? Kwamba waachane na imani hiyo? Kwamba wako sehemu isiyowafaa? Kama unaona (wewe kwa maono yako) kwamba mtumishi wa Mungu huyu anawadanganya au anaenda kinyume na matendo au maagizo ya Mungu,wewe binafsi usiende kusali katika kanisa lake,na wale wanaoona yuko sawa basi waache maana hawajavunja katiba ya nchi.
Kwa ule upande wa pili naona kama umeanika hata kilichokuwa kimefunikwa...

Asante ngosha ngw'ichane.
 
Huu mchezo wa watu wa kwa mwanamalundi kuparurana una raha yake. Hii unaweza ita mwanamalundification. Hahahaha..... ila hasira aihitajiki, lete raha!!
 
Pascal nadhani keshapewa cha juu, kama mnakumbuka ndo aliyeleta awali hizi tuhuma akizitoa kwenye page ya Mange Kinambi leo anasema ni uzushi, kwa mantiki hiyo Pascal ndo mzushi namba moja
Pasco ni msahaulifu mkubwa pia njaa yake ni hatari maana imemfanya ajitoe fahamu kwa kiwango cha kutisha, nadhani alitengeneza mtego awali sasa mtego wake umenasa na yupo anakula pesa za Daud Albert kiulaini na kutumia akili ya Steven Nyerere.
 
watu hawa msingizii asee kwa kuwa kamwaga ugali sasa watu wameamua kumwaga mboga.hivi kwn mnadhani hakuna watu waliosoma na makonda tangu awali.au wamekufa woote??vipi kitaani aliokuwa anaishi nao wamekufa woote??

acheni ulofa watu wanamjua vzr tuu.huwez kuwafanyia vbya watu wakakuangalia tuu.tanzania ya leo sio ya jana watu wameenda shule mpk kero
 
Naunga mkono hoja kwa 1000% kwa sababu makonda ndiyo alianza vita, cha ajabu eti Gwajma kaamua kujihami lakini wapo watu hawataki Gwajma ajihami!
 
Duniani tumegawana ushabiki wapo wa hiki na wengine kile,kikubwa tuvumiliane, ukichoma pia uvumilie ukichomwa... Dunia inaendelea lakin
 
Hoja za kitoto! Naona umezaliwa kwenye familia ya watoto wa kiwango cha chini. Pole kama watoto wako wana hoja mbovu. Watoto wangu wako powa! Shida yako ni nini? Makonda aache mambo ya madawa? Makonda amuache Gwajima (mtumishi wa Mungu)? Makonda afukuzwe kazi?

Kila wakati fikiria usisubiri Gwajima afikiri kwa niaba yako. Makonda kwa nafasi yake alistahili kupambana na madawa ya kulevya. sasa huyo Mtumishi wa Mungu naye kazi yake ni kukamata vyeti feki? Shit!
 
Tatizo lako ni kanjanjaaaaaaaaaa at work umelipwa ngapi
 
Kazi ya Ukuu wa Mkoa siyo ya kutuma application hata kama hujui kusoma wala kuandika unaweza kupewa hiyo nafasi, kazi hii inataka hekima, busara na maarifa, wazee wanaweza kutumia busara na kumaliza hili bifu kwa amani.
Hakuna MTU anayepinga kuteuliwa kuwa RC....hapa watu wanataka kujua Daudi Bashite ndio Paul Makonda?Baba Askofu nipe Mimi hivyo vyeti niviweke mtandaoni Niko tayari kuface consequences...
 
Ndugu yangu uandishi ya Paskal unahitaji utulivu wa akili ndipo umweelewe,wewe unaweza ukafikiri kwanda anamponda Gwajima lakini kumbe sio hivyo.

Hana haki ya kumwita mtu nabii wa uongo!!!! HANA hiyo haki. Kwa ubinadamu kabisa kwa shutuma alizopewa huyu Mchungaji, kama si za kweli ni lazima akasirike. Katengeneza Jina na heshima yake mda mrefu. Mambo ya Imani yake mimi hayanihusu.
 
Kwa mambo ya kiroho Gwajima Yuko juu zaidi ya Rais kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu kwa mambo ya kiutawala wa dunia Rais Yuko juu zaidi ya Gwajima.
 
PASCAL naona unaingia porini,jadili hoja iliyopo mezani acha kudadili pointi moja tu,Mkuu amtumbue ASAP asizidi kuchafuka.Tunamuamini mkuu kwa kazi yake nzuri anayofanya ya kulinyoosha taifa kumbe kuna watu wanapindisha kwa manufaa yao.Hatukuyajua haya kabla sasa tumeelewa pasi na shaka sababu ya kuwaandana watu kama Ngwajima.
 
kama huna hoja kaa kimya....KIUMBE maana yake: (kwa mujibu wa kamusi) chenye kuumbwa na chenye roho, kama: binadamu, mnyama, ndege, samaki na wadudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…