Pre GE2025 Mchungaji Kimaro: Uchumi unaanguka sababu wenye akili hawatumiwi. Wenye akili siyo tishio kwenye nafasi zenu, watumieni kwenye uzalishaji

Pre GE2025 Mchungaji Kimaro: Uchumi unaanguka sababu wenye akili hawatumiwi. Wenye akili siyo tishio kwenye nafasi zenu, watumieni kwenye uzalishaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Mbunge wa Jimbo la Hai, Msikilize baba mchungaji, kuna ujumbe wako.

"Kwanini taasisi zinakufa? Kwanini Uchumi unaanguka? Kwanini kutokuzalisha? Ni kwasababu hautumii wenye akili! Namna ambavyo unaweza kuzalisha ni kutumia wenye akili. Sasa ukishaona kila mwenye akili kwako ni tishio (threat), ukimuona kila mwenye akili kwako ni pigo, ukimuona unashtua, HAPANA. Mtumie mwenye akili akuweke kwenye kiti sawa sawa.

"Kwasababu Yusuph hakuwahi kumpindua Pharao, lakini Pharao aliendelea kutawala wananchi wenye chakula, na wananchi wakishakula wakiwa na maisha yao, we piga siasa zako utakazotaka hawahangaiki, ila huwezi kumtawala mwananchi mwenye njaa. Ndio kile kinachoendelea nchi Jirani za Afrika, tena Afrika Mashariki.

"Mtu akiwa na njaa hatawaliki, nak ama una mtu mwenye akili anayeweza kusababisha chakula kiwepo mtumie ili ubaki kwenye kiti. Mwenye akili hana mpango na kiti! Mwenye akili anawepo kusaidia watu wakae kwenye kiti, mwenye akili haitaji siti ya kudumu! Hakuna mwenye akili anahaingaika na siti ya kudumu hata siku moja.

"Sasa kutana na mjinga anayelinda kiti, mjinga anayelinda kiti anaua wenye akili akiamini atakaa! Hatakaa kwasababu wenye njaa watamtoa. Wenye njaa wameingia bungeni wakala chakula cha bunge! Watu wako serious hivyo wakiwa na njaa.

"Kwa kumaliza ningeomba sana siyo Tanzania tu, Afrika yote tukubali kutumia wenye akili. Makampuni, ninyi ma CO, tumieni wenye akili, hata kama ni darasa la saba ana akili anaweza kuchangia na kusababisha uzalishaji kwenye makampuni, taasisi, nk, uzalishaji unafanywa na wenye akili."


 
Back
Top Bottom