Mchungaji kortini akidaiwa kumuua dereva kwa kukusudia

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Ernest George (37), amepandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia ya dereva, Majuto Seif.

George, ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (T.A.G), maarufu Mchungaji George amesomewa shitaka katika kesi ya mauaji namba 19830/2024, leo Jumatano Julai 17, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Amesomewa shitaka hilo na Wakili wa Serikali, Evance Kaiser mbele ya hakimu, Stella Kiama.

Mchungaj_mauaji.jpg

Kaiser amedai mshtakiwa na wenzake wanne ambao hawakuwapo mahakamani walitekeleza mauaji ya dereva huyo Juni 27, 2024 katika eneo la Lugeye wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.

Anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha vifungu vya 196 na 197 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 na marejeo ya mwaka 2012.
 
Ilikuwaje mkuu?
 
Nadhani ndio lile tukio la aliyeuwawa na kuporwa gari Toyota Ractis,huyu Mchungaji atakuwa aliuziwa hilo gari hivyo kakamatwa nalo

Nchi yetu mbona jinai husomba waliomo na wasiokuwemo? Huu ni ujima. Kwa nchi nyingine si rahisi kuungwa katika kesi kama hii kisa tu umeuziwa gari ama kifaa chochote. Ni lazima kuwe na ushahidi kuwa uliagiza wafanye tukio ili wakuuzie, wanunuzi wengi kawaida hawajui historia ya bidhaa used wanazonunua. Tunahitaji mageuzi ya upelelezi jinai.
 
Au alikua anakula mali za mchungaji? Wivu wa mapenzi?
 
Ernest George (37), amepandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia ya dereva, Majuto Seif.

George, ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (T.A.G), maarufu Mchungaji George amesomewa shitaka katika kesi ya mauaji namba 19830/2024, leo Jumatano Julai 17, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Amesomewa shitaka hilo na Wakili wa Serikali, Evance Kaiser mbele ya hakimu, Stella Kiama.

Kaiser amedai mshtakiwa na wenzake wanne ambao hawakuwapo mahakamani walitekeleza mauaji ya dereva huyo Juni 27, 2024 katika eneo la Lugeye wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.

Anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha vifungu vya 196 na 197 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 na marejeo ya mwaka 2012.
Kuna registry zina kesi nyingi!!! RM mwanza hii 2024 zimefika 19,830.Hapo hata overtime zina paralyse
 
Kawaida yao ... Kumbuka issue ya Albino
 
Back
Top Bottom