Mchungaji Lwakatare Arudisha Yatima 250 Kwao

- One more time, hii habari ni ya kweli?

confirmed, now lies the second task...coordinating the next phase, life continues..all was needed was more information, It seems Tujisenti has more info, will be intouch. see thats how JF works, post a concern and maybe someone has info...ngonjera ni interpretation yako tu, which is also fair since this all opinions are welcome.
 
Tatizo hapa linakuja kwa vile Lwakatare ame declare kwamba yeye ni mtumishi wa Mungu.Kama angekuwa mtu wa duniani au wa kawaida hakuna mtu ambaye angejali.Mtu wa Mungu si hiari kuhudumia yatima na wajane,ni amri kutoka kwa Mungu.Sasa kitendo alichofanya kama ni kweli ni kinyume cha agizo la Mungu.Mungu anapompa mtu mali au chochote hasa mtakatifu,hampi kwa ajili yake tu ila anampa kwa ajili ya wengine pia.Yule mtu anakuwa kama mfereji wa kupitishia maji, lakini wanaokunywa ni wengi.Kwa hiyo kwa mtazamo wa kitakatifu, alichofanya Mchungaji Lwakatare ni makosa,lakini kwa mtazamo wa mtu wa kawaida hakuna tatizo.

 

Heee unaosha jina!

Still is non of ur business, kwani alipowachukua hao watoto na kuanza kuwasaidia alitoa ahadi kwamba atawasaidia hadi watakapokufa? (hilo litakuwa tatizo kama kweli), na jej, mbona unampangia nini afanye na mali zake alizotafuta kwa jasho lake? au ndio unampangia huruma yake kwamba iendelee mmbele kidogo isiishie hapo, basi ipokee wewe hiyo huruma uendelee nayo. Msaada anaotoa mtu siku zote ni hiyari na utaishia pale muhusika anapoona inafaa, cha msingi muombee kwa Mungu apewe zaii ili aweze kuendelea kuwasaidia.

for the time being ninakuomba uwachukue wewe hao watoto uwalee kama alivyokuwa anawasaidia yeye ili wasiteseke. na Mungu atakuzidishia kama alivyomzidishia Lwakatare.
 
Nimepata Habari kwamba mchungaji Lwakatare ameamua kurudisha Yatima 250 makwao kwa kisingizio ....

Mwana habari,
Mbona neno KISINGIZIO linaleta mashaka kwa hoja yako?
kama unahitaji kupata ukweli wa jambo, ni vema usi bebe mawazo egemezi kwenye mtazamo wako.
Mimi sijui ukweli wa hizi tuhuma zako.
 
Jamani ngoja nitotautiane na wale wote mnaomtetea Mama Lwakatare or Mchungaji Getrude Lwakatare!!!!! Mimi si mtaalam wa dini wala vifungu vya bibblia ila ninachoelewa kuna kifungu kinachosema katika biblia kuwa ... dini safi ni ile ya kuwahudumia yatima na wajane, Na Mungu mwenyewe amesema yeye ni mume wa wajane na baba wa yatima. Mwenye kujua kifungu hicho cha biblia lete citation hapa, nitashukuru.

Kwake mama Lwakatare, Mungu ameshampa utajiri wa kutosha kupitia miradi yake mingi ikiwemo shule za msingi, sekondari, vyuo na of all mafungu ya kumi na sadaka kutoka kwa matajiri wa kanisa lake ambazo hazina hata kodi kama ilivyo shule zake. Ni mjanza sana amejua mahali pa kuwekeza!!!!! Sasa basi inakuwaje ashindwe kulelea yatima 250 ili Mungu aendelee kumbariki???? Anaweka maslahi yake mbele zaidi kuliko hawa watoto. Anao uwezo wa kuwatunza na kuwasomesha!!!!!!! Mungu amempa hiyo nafasi na aitumie kwa ajili ya jamii na si kutaka kuangalia maslahi yake.

Nina ndugu yangu alikuwa anasoma kile Chuo cha St. Mary's cha Ualimu Tabata!!! Ni feki na mitihani yake ni ya feki pia!!!! Kuna walakini sana pia hata namna ya kuendesha shule na taasisi zake nyinginezo!!!!!Maisha ni magumu sana hata kwa wafanyakazi wake, ndo maana wengi wa waalimu walishaondoka na sasa aliamua majuzi kupunguza wafanyakazi maana standard ya huduma zake imeshuka so demand is down na inabidi baadhi ya streams za mashule yake zifungwe!!!!! Wazazi wengi wamehamisha watoto wao maana pale is business as usual now, kiingereza kwa sana but no substance in the head!!!!!

Mimi binafsi nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu uadilifu na ulokole wa huyu mama!!!!! Is she really a born again christian!!!????? Is she using ulokole kuficha njia zake za kupata utajiri?????!!!!! Ikumbukwe pia akina Japhet Lema wa Njake Enterprises na akina Jonson Lukaza ni walokole wanashiriki kutoa michango mikubwa makanisani na kutoa shuhuda za mafanikio kifedha na kiutajiri kumbe ni wezi wakubwa sana kupitia EPA na ujanja mwingineo!!!! Kwa mantiki hiyo sikubaliani na mlokole yeyote duniani hapa, kama mtu ni mlokole ni yeye na Mungu wake period. Dini au makanisa mengi ya siku hizi ni biashara tupu. Wachungani wengi wanakuwa karibu sana na wale waamini wenye pesa, ukikosa kanisani mara moja tu mchungaji anakupigia simu ila kwa wale wasio na uwezo hakuna hata mzee wa kanisa anatumwa kuwatafuta wanapokua hawaonekani makanisani. Yaani wakati mwingine wale watoa sadaka na mafungu ya kumi kwa wingi wanaketishwa viti vya mbele maana hao ndo pia wanavalia vizuri ili inapochukuliwa picha ya video basi kanisa linaonekana liko smart sana!!!!!

Mungu akitupa uhai tukaishi basi mwisho wa mama Lwakatare hautakuwa mzuri sana. That is my prediction and do not ask!!!!!!!?????? Yule ni mfanyabiashara na hataki kutoa senti yake bure. Ndo maana ameamua kuwarudisha wale watoto, pengine kuna proposal aliandika kwa ajili ya orphanage na alipokosa mipesa akaamua kurudisha watoto makwao, vinginevyo anao uwezo tosha wa kuwatunza na kusomesha watoto maskini kama wale. Yeye hapendi maskini, anapenda matajiri ambao wanampa mafungu ya kumi na sadaka nene.

Namshauri achukue kioo ajitizame huku akiliita jina la Yesu akimaanisha, then awatizame wale watoto wanavyorudi katika mazingira magumu then aseme na huyo Mungu au Yesu wake kama kweli anafanya sawasawa.

Kuna wale mliosema eti kulea Yatima ni jukumu la Taifa!!!!??? Imenishangaza sana. Taifa lipi???? La Tanzania au Magharibi au Asia, au Ulaya au wapi????!!!! Taifa kama taifa halifanyi direct role ya kulea makundi ya watu bali lina facilitate. Na kufanya hivyo inawezekana kama tu Taifa lile ni dedicated kwa kazi hiyo au pia linajali kiasi gani na pia kama resources zipo. Ninachojua taifa linarusu kuwe na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuhudumia makundi mbalimbali ya wahitaji au disadvangaged social groups!!! Kama ni taifa lenye uwezo lina subsidize taasisi hizi through kodi na pengine yale matajiri huenda wanatoa ruzuku (mtanisaida hapa kwa wale mnaoelewa kama nchi tajiri zinasaidiaje yatima na makundi hitaji), pia kupitisha proposals zote kwa donors through wizara inayohusika na masuala hayo. Kwa maana hiyo basi taasisi hizi zinaendeshwa na management and administration ya private ila tu serikali inawatambua na kuwasaidia pale inapohitajika na kama uwezo upo. So we need watu dedicated kuanzisha hizo orphanage centers na si kuzianzisha na kuzitumia kama vitega uchumi kupitia misaada na ruzuku kuingia mifukoni mwa viongozi???? Tatizo letu Watz matapeli tuko wengi sana.

Nalipongeza kanisa Katoliki ndilo pekee ambalo limeweza kusaidia watoto yatima katika centres zao, pia masista wa kikatoliki and they are dedicated to this. Yaani wana moyo wa kuwalea na kutunza yatima sema yatima kwa sasa ni wengi sana na uwezo kimiundombinu na rasilimali nyingine ni mdogo.

Hivyo ndugu zangu, nisamehe sana kwa kuwa nimepingana na Lwakatare na wote mliomsapoti. Sorry Field Marshal ES et al...
 

.........!!!!

Ndugu zangu mliotaka uthibitisho bila nyinyi wenyewe kutembelea miradi hiyo mtanufaika na contribution hii ya NDg Maane, it is straight from the heart.
 
Ninachokiona hapa kuna watu wanakuwa na mapenzi binafsi na mtu fulani,inapotokea jambo likawekwa hapa hadharani kuhusiana na mtu huyo,watu watataka ulete uthibitisho na kukushambulia.Kwa mtu anayehitaji uthibitisho sidhani kama anatakiwa kuonyesha alikoegemea kabla ya kupata uthibitisho aliouhitaji.

Inawezekana kabisa habari hii ikawa na ukweli ndani yake! sipendi kumnyoshea kidole Mchungaji Lwakatare lakini nimewahi kusikia habari kama mbili zinazomuhusisha na kuwazima watu pesa zao. Sasa nikijumlisha 1 na 1 napata mbili. Kwangu mimi lolote linawezekana hasa pale mtu anapokuwa anapenda sana pesa na kujilimbikizia utajiri uliokithiri! mtumishi wa mungu haitaji utajiri wa kupindukia badala yake anahitaji utajiri wa kuokoa nafsi za watu waliopotea ili waweze kumuona mungu siku ya mwisho.

Asante
 
Kama aliwakusanya mayatima hao na kuwatumia kupata misaada kutoka kwa wafadhili, basi atakuwa anafanya makosa makubwa sana. Ila kama huwa anatumia pesa yake mwenyewe kuwalea na kwa sasa hivi anaona kaishiwa, mie sioni tatizo.


Fadhila zisizidi uwezo
 
Inawezekana kabisa habari hii ikawa na ukweli ndani yake!

- I am out of this thread! Mpaka itakapothibitishwa kua habari hii ni ya kweli, maana namuona njemba mmoja kwenye hii thread anafikri ana akili sana kuliko sisi wengine wote humu, ni waste of time na space pia!
 
ni pesa zake. alee yatima, au afanye chochote ni uamuzi wake. tunamshukuru hata kwa kuwalea kwa muda wote huo. lakini nafikiri akijenga university ndio itakuwa safi zaidi, kwasababu hiyo itakuwa na faida kubwa zaidi tz na kwa watu wengi zaidi tz. wewe unayelalama, mwenye wivu na chuki, umelea yatima wangapi? hivi hauoni aibu mwenzio kalea hadi kufikia 250 kwa hela yake, halafu wewe unataka kumpangia maisha? kama ameshindwa kwa ukata wa pesa na anataka kujenga university ili araise money si uamuzi wake? wewe unafanya naye biashara?

wewe unayesema pesa ni shetani, yanakuhusu nini? duniani hapa, watu wenye wivu wanabakigi masikini tu hivyo hivyo, kwasababu badala ya kushugulikia maisha, wanashugulikia mambo ya watu. badilikeni jamani. na nyie sasa mumpokee kulea hao, mwenzenu amechoka. yeye pia ni binadamu. unamdai hela lwakatare kwani? yanakuhusu nini? si ushukuru hata hapo alipfikia?
 
- I am out of this thread! Mpaka itakapothibitishwa kua habari hii ni ya kweli, maana namuona njemba mmoja kwenye hii thread anafikri ana akili sana kuliko sisi wengine wote humu, ni waste of time na space pia!

Mimi ndiye niliyeandika sana!!!! Ninao muda wa kufanya hivyo pale inapobidi kusema ukweli ninao ufahamu. Swala la akili sana hizo ni inferiority complex, halinihusu mimi. Hapa we dare to talk open, we have democracy na si kutishana hapa. Yes, wewe ni mdau hapa siku nyingi, nakuheshimu nawe niheshimu pia. Ni kipimo kipi unatumia ku judge wenzio kuwa wana akili au hawana????? Mods ni vema kuwakumbusha wengine hata kama ni wakongwe wa hii forum waheshimu sisi tunaoonekana tukichangia tuna akili sana au kutudharau kwa sababu ya ugeni wetu au tuseme ujunior wetu. Hapa kwenye forum haijalishi umeingia lini, kuna wau ambao wakiingia leo michango yao ni mikubwa kuliko wale ambao wapo tangu awali, registration date is not sufficient to prove intelligence ya mtu au uzoefu alio nao katika masuala ya kijamii. Humu ndani yawezekana mwanangu ni member, na inawezekana kajisajili 5 years ago na mini mwaka jana tu. Haiwi kipimo kuwa mwanangu huyo anafahamu mambo mengi kuliko mimi. Pia atueleweshe tunatakiwa tutumie space kiasi gani katika kuchangia. Hata Yohoo. com space ni kubwa these days!!!!! Tuheshimiane kaka/dada yangu. Huwa ninakuheshimu sana na michango yako positively or negatively kwenye issues na si lazima kukubaliana na kila kitu member anachopost hapa. Kwa ukweli na uwazi ungenitaja tu jina MAANE. Nina amani moyoni katika mchango niliotoa hapo juu kuhusu ninachokifahamu kwa miradi ya Mama Lwakatare sikumtukana mtu wala kusingizia, nimesema ukweli. Huwa sina tabia za majungu hata ukienda back to all my postings utakuta hilo. Sitapenda kulumbana wala kutukanwa kwa sababu nimekujibu, si tabia yangu. Ukiwa wazi katika maisha utaepuka mambo mengi sana hasa magonjwa. Mimi mi mtu mzima. Thank you.
 
Hivi ktk Crisis Situation Serikali haiwezi kuombwa kuchukua jukumu kwa kutumia pesa ya kodi? iwe kama bail out kuliko kuwarudisha hawa watoto makwao?

kama kila mtu angefanya anayoyafanya Lwakatare hapa tz, basi tz ingekuwa mbali sana. pesa za rwakatare wala si nyingi. ni bilion kadhaa tu wala hatishi. hapa tz kuna watu wenye bilion zaidi ya mia moja na kuendelea, lakini hata hawaongelewi. huwa hawawezi hata kutoa sadaka kwa yatima au hata kwa kina matonya barabarani. wanaweza wakatoa million mia moja ili watu waingie yanga bure uwanja mzima mpirani. kina lowasa, kina mawaziri fisadi wote hao. kina maraisi wote hao akiwamo hata kikwete mwenyewe. wahindi ambao kwa kusema kweli ndio wezi wa nchi hii wakubwa ambao wamekuwa wakiwa kama kivuli cha viongozi wa nchi, viongozi wanaiba pesa, wanawapa wahindi, wahindi wanajenga viwanda etc, na inaonekana kama kiwanda cha muhindi kumbe ni ubia fulani. kuna watu wenye hala sana,lakini hata hawajali yatima hata mmoja. yeye rwakatare kwa vishule vyake vichache, ameamua kuchukua badhi ya yatime, walipomshinda kulisha aliamua kuwarudisha.

hiyo sio aibu kwake, ni aibu kwa selikali, kwasababu selikali imeshindwa kusapoti hata wale wanaosapoti watu. selikali yetu imeaibika sana, haijavaa hata nguo, yaani iko uchi wa mnyama. naomba mwacheni huyu mama, msemeni kwa lingine lakini sio kwa hili. au ni kwasababu mchungaji?

ninyi mnaoongelea mafungu ya kumi, mnajua namna yanavyotumika? hivi mnafikiri hizo shule zina pesa nyingi basi? ni za utajiri wa kawaida tu ila sio utajiri wa kutisha.
 
FMES
Unatushitua kidogo, nimefuatilia hii thred toka imetoka kila unapocomment wewe ni kumtetea tu mama huyo, KULIKONI. Wanasema KUPENDA hupofua na chuki hupofua, wewe uko wapi????????????????.
Kuna mambo hayahitaji kuulizwa, mwenye macho haambiwi tazama na masikio haambiwi sikia.
Kuna vitu ni vya msingi tu, vya shule au binaadamu. Kwa vile mada ni nzito ladba tuchangie hawa watoto wanakwenda wapi baada ya hapo??????????
Tujichunge KUTOANZISHA KITU TUSICHOWEZA KUKUMALIZA.
Nadhani tunafahamu kuwa misaada mingi inatoka nje ili kusaidia baadhi ya wenye shida, bila kuonyesha hupati, japokuwa wengi wa hiyo missada inatumika kuganga njaa ya waliojifanya wanataka saidia kama hao watoto............sasa
 
Ni kweli wafadhili wake ULAYA wameanguka kwa sababu ya Credit Cruch na mchungaji hakuwa na mpango mbadala, embu na sisi watanzania tujadili jinsi ya kuwasaidia hawa yatima, wakati mwingine tuwe tunajadili na ufumbuzi siyo kulalamika tu na kushutumu

hongera mama lwakatare hata kama kuna matatizo you have done something out of nothing...
 

Alipowachuka alisema watasoma bure mpaka University!!! Alipoamua kuwarudisha hakuwajulisha waliowaleta. Angetoa taarifa mapema tungewatafutia shule mapema.
 
Mwana habari,
Mbona neno KISINGIZIO linaleta mashaka kwa hoja yako?
kama unahitaji kupata ukweli wa jambo, ni vema usi bebe mawazo egemezi kwenye mtazamo wako.
Mimi sijui ukweli wa hizi tuhuma zako.

Mch Lwakatare alipoulizwa kwanini ameamua kurudisha watoto kwao hilo ndilo jibu alilotoa kwamba watoto wengine wana ukimwi wengine wanaumwaumwa.Nafahamu badhi ya hao watoto ni wazima wa afya
 

Mungu huyo wa yatima ndiye huyo atakayomhukumu. Aliamua mwenyewe kutunza yatima sasa kawaacha kwenye mataa ile ajenge chuo ki kikuu. Tamaa kwa jina la Yesu!!
 
- I am out of this thread! Mpaka itakapothibitishwa kua habari hii ni ya kweli, maana namuona njemba mmoja kwenye hii thread anafikri ana akili sana kuliko sisi wengine wote humu, ni waste of time na space pia!

Hii habari ni ya ukweli kabisa kama wewe hutaki kwamini shauri yako
 

- Mkuu Maane, heshima mbele sana kaka, hapa umenishangaza sana kwa sababu nimehesabu ndani ya hii thread wewe umechangia mara moja na hii ya pili tu kwa jina la Maane, sasa naomba nikuulize hivi haya maneno yote hapo juu ni juu ya nini hasa na wewe ndio kwanza umechangia mara moja tu na hii ni ya pili? Sasa unaona unavyojiweka wazi mwenyewe kuwa una something to do sio tu na inferior complex ila hata maana ya quote yangu uliyoi-quote wewe mwenyewe?

- I mean pili pili iko shambani wewe imekufikaje mkuu? Au inakuhusu vipi? Mimi siwezi kumtetea huyu mama as a person kwa sababu simjui ingawa ninajua some of mapungufu yake, lakini hayajafikia kuwa tatizo kwa taifa sasa unataka nini kwamba tusiulize ukweli wa habari yako?

- Sio mara ya kwanza unaleta huu mchezo wako kwamba ukianzisha topic lazima wote tukubali tu, otherwise utajaribu kuzunguka zunguka as if sisi wengine wote hapa ni wajinga, unakumbuka ile topic ya Kikwete na kutojiamini? Hivi hivi ukaleta ukali wee na maneno mengi ya kashfa kwa sababu nimetofautiana na mawazo yako vipi mkuu kwa nini msianzishe forums yenu maana mko wengi sana humu ndani kwamba ni lazima wengine tukubali tu mawazo yenu, WHY?

- Nimekuuliza time and time again ukweli wa hii habari, unajaribu kunizunguka na ujanja wako mwingi badala ya kujibu swali, what quote yangu has to do na wewe Maane na sio wengine wote kwenye hii thread? Unaweza kunijibu hili swali kama wewe ni mkweli kama unavyodai? Acha utoto mkuu wewe uko wazi sana jina lako la kweli ni Maane? Wewe huwaoni walio wazi humu kina Mkandara na Kitila?

- Tarehe yangu ya kujiunga hapa inahusu vipi na mawazo yangu na wewe na mawazo yako? Halafu eti ndio unataka kuongelea inferioritism? Kweli mkuu unaelewa maana ya hili neno au mnakurupuka tu? Acha hiz bro kama huwezi kuleta ukweli wa habari yako wewe endelea na mawazo yako, lakini usitulazmishe wote hapa tuwe tunakubali tu kama wajinga, hakuna mtoto wako hapa wote sisi ni watuwazima, huna ukweli huna right to speak wala kumlaumu yoyote anayeuliza,

Kwenye hii habari simply huna ukweli wa mada na kumhusu huyu mama, sisi hatuko hapa kuchafua majina ya viongozi bila sababu, sio tabia yetu hata siku moja mkuu, samahani kwa kukukwaza lakini umenishanganza sana kwamba from all the people kwenye hii thread wewe tu tena na mchango mmoja ndio umekwazika na kunirushia maneno ya chooni, ni lazima nikujibu bila ya kujali tarehe yako au yangu ya kuingia hapa maana it has nothing to do kabisaaa na mawazo yangu, ingawa inaonekana mawazo yako hutengenezwa na tarehe ya kuingia hapa, I am sorry sio na yangu!

Sauti ya umeme - FMES!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…