Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Akiwa katika Mahakama ya Shanzu ambapo shauri dhidi yake na washirika wake linatajwa, Paul Mackenzie alipiga kelele akiitaka Mahakama iwaue kisha miili yao itupwe Mto Yala, akidai haki zake na za Washtakiwa wenzake 15 zilikiukwa wakiwa Gerezani, baada ya kunyimwa dhamana
Amemwambia Hakimu, "Nimekaa Siku 2 bila Kula na Kuoga kwa sababu nimefungwa 24/7 kwenye chumba chenye giza. Mamlaka ndiyo inaelekeza nitendewe hivyo, najiuliza ni nani ataniokoa? Ikiwa umetuchoka na hutaki kutupatia Haki za Msingi unaweza kutuua na kutupa miili yetu katika Mto Yala. Baada ya yote, sisi sote tutakufa siku moja. Mahakama hii inahitaji kunisaidia kwa sababu ninateseka"
Mchungaji Paul Mackenzie na wenzake wanazuiliwa kuhusiana na vifo vya watu 425 akidaiwa kuwashawishi kufunga hadi kufa huko Shakahola, huku zaidi ya watu 600 bado wakiripotiwa kutoweka
Chanzo: Citizen Digital