Mchungaji Matsai: Watanzania tunatambuana kwa Utanzania wetu na siyo Dini zetu, serikali ijenge fly over Jangwani!

Mchungaji Matsai: Watanzania tunatambuana kwa Utanzania wetu na siyo Dini zetu, serikali ijenge fly over Jangwani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mchungaji Matsai wa Kanisa la KKKT Kimara amewataka watanzania waendelee kuwa wamoja kwani nchi yetu haina dini ila watu wake ndio wana dini.

Matsai amesema hayo mbele ya Waziri wa uwekezaji Prof Kitila Mkumbo na Naibu Spika Dr Tulia Ackson aliyeshiriki ibada Kanisani hapo.
Kadhalika mchungaji ameiomba serikali ijenge daraja la juu pale eneo la jangwani kwani nyakati za mvua barabara ile huwa haipitiki kabisa hivyo anaamini kabisa Rais Magufuli atatenda.

Mwisho mchungaji Matsai amewataka mawaziri wote wakafanye kazi kwa mujibu wa viapo vyao na wasisikilize mambo ya mitandaoni kwani kidini tunatambuana misikitini na makanisani lakini siyo kwenye majukumu ya serikali.

Source Upendo tv

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Mchungaji Matsai wa Kanisa la KKKT Kimara amewataka watanzania waendelee kuwa wamoja kwani nchi yetu haina dini ila watu wake ndio wana dini...
Wafuasi wa Moody sijui kama watamwelewa.

Wao dini kwanza mengine baadae.

Ni wazalendo zaidi kwa dini kuliko kwa nchi na serikali.
 
Back
Top Bottom