BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
DEMOKRASIA: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amesema ili kupata Viongozi wanaoweza kukabiliana na CCM, chama hicho kinapaswa kutumia njia ya Midahalo ya Wazi kupima uwezo wa Wagombea
Msigwa ameeleza hayo wakati akizungumza na Wanahabari na kusema "Napendekeza katika ngazi ya Taifa kwa mfano kunatakiwa kuwe na Midahalo si chini ya Mitano kwenye Kanda ili watu wajue huyu Kiongozi anaweza kukabiliana na CCM?"
Amesema Wagombea hawapaswi kujificha kwenye koti la Chama wakati ili chama kiweze kushinda katika Chaguzi kinapaswa kuwa Mgombea Anayekubalika, Mwenye Agenda, Mipango na Fedha
Kauli za Msigwa zinakuja siku chache baada kutangazwa matokeo ya Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti Kanda ya Nyasa ambapo Joseph Mbilinyi alishinda nafasi hiyo dhidi ya Msigwa.