DEMOKRASIA: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amesema ili kupata Viongozi wanaoweza kukabiliana na CCM, chama hicho kinapaswa kutumia njia ya Midahalo ya Wazi kupima uwezo wa Wagombea
Msigwa ameeleza hayo wakati akizungumza na Wanahabari na kusema "Napendekeza katika ngazi ya Taifa kwa mfano kunatakiwa kuwe na Midahalo si chini ya Mitano kwenye Kanda ili watu wajue huyu Kiongozi anaweza kukabiliana na CCM?"
Amesema Wagombea hawapaswi kujificha kwenye koti la Chama wakati ili chama kiweze kushinda katika Chaguzi kinapaswa kuwa Mgombea Anayekubalika, Mwenye Agenda, Mipango na Fedha
Kauli za Msigwa zinakuja siku chache baada kutangazwa matokeo ya Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti Kanda ya Nyasa ambapo Joseph Mbilinyi alishinda nafasi hiyo dhidi ya Msigwa.
Msigwa ana hoja nzito na ya maana! midahalo inasaidia wagombea na wapiga kura kwa pamoja
Pili, Msigwa alilalamikia msimamizi J.Mrema kabla ya kura. Lakini pia si kuna taratibu zinazoendesha uchaguzi?
Ikiwa ni hivyo, kwanini Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa CDM hawakuona umuhimu wa kutengeneza mazingira mazuri ya kufuata taratibu na kanuni zao ili kukiweka chama chao pamoja
Hili jambo lina tatizo kubwa, kimya cha Katibu Mkuu ambaye ni mtendaji na Mwenyekiti anayepsawa kuunganisha chama chao ni tatizo. Hata kama Msigwa hana hoja lakini mazingira tu yanamjengea hoja.
CDM wanapaswa kusafisha safu yauongozi wa juu, kuna tatizo kubwa sana
Humtendei haki Msigwa,sasa kama ameona kuna ukiukwaji wa kanuni na ameonewa ulitaka akae kimya tu? Lazima watu tuelezane ukweli haya mambo ya kufumbia macho
maovu yako CCM tu.