PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 969
- 1,055
Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa zamani wa Iringa mjini na waziri kivuli wa maliasili na utalii ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Nyasa amesema kuwa pamoja na Tofauti zao za kisiasa na kupishana kwa mambo kadhaa ya hapa na pale, jambo moja muhimu ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anapaswa kuwafanyia WATANZANIA na likabaki kama LEGACY kwake basi ni kuiokoa Hifadhi hii ya NGORONGORO ambayo inazidi kuteketea kutokana na ongezeko kubwa la watu, ongezeko kubwa la mifugo, ongezeko kubwa la Nyumba zisizoendana na uhifadhi ikiwemo ujenzi wa Maghorofa, ujenzi holela na hali mbaya ya maisha inayowakuta wananchi wanaoishi eneo hilo huku wale wanaojinasibu kuwatetea wakiishi maeneo nyeti na mazuri yenye huduma zote za msingi jijini Dar es salaam
"Hatuwezi kuwa na wachoyo wachache, ambao ng'ombe zao, biashara zao ziwe muhimu kuliko Ngorongoro inayoingizia mabilioni ya fedha zinazosaidia kupeleka huduma kwa jamii" amesema Mchungaji Msigwa
Mwalimu Nyerere alituachia urithi huu, ni wajibu wetu kuutunza, Serikali ya CCM imeshindwa kuutunza, na ndio maana tunaipinga na tunataka kuiondoa madarakani, haiwezekani watu wanajenga majumba hifadhini, wanazidisha mifugo nakadharika na CCM WAPO TU aliongeza Msigwa.
OKOA NGORONGORO