Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mchungaji Peter Msigwa aliyekihama Chama Cha Chadema hivi karibuni na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, akiwa mstari wa mbele kuipigia chapuo CCM huko mkoani Iringa, asubuhi hii amekuja na hoja binafsi wakati huu ambapo Kamati kuu ya Chadema inaketi kufanya tathimini ya Uchaguzi huo uliokuja na matokeo ambayo kimsingi hayatoi picha nzuri kuelekea hatma ya vyama pinzani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mch. Msigwa katika hoja yake anaikumbusha Chadema kuwa huwezi kujenga Chama cha siasa bila kuwa na sera za wazi na zinazoeleweka kwa wafuasi wako na wale unaowashawishi kuwa wafuasi wako.
Anasema Ukosoaji sio sera ya Chama cha siasa kinachojitambua na bahati mbaya ukiegemea kwenye kukosoa pekee chama kilichopo madarakani, ipo siku vyama pinzani vitakosa ajenda za kukosoa kutoka kwenye Chama tawala na matokeo yake huo ndio utakuwa mwisho wa vyama hivyo.
Mch. Msigwa katika maelezo yake anahoji ni Watanzania wangapi wenye kufahamu Msimamo wa Chadema kwenye masuala ya Kikodi, Sera za kigeni, Sera za Ulinzi wa Taifa, uhamiaji, haki za wafanyakazi, mazingira na kadhalika. Mch. Msigwa anasema Chadema ile anayoifahamu inajulikana zaidi kwa umma kwa kile inachokipinga kuliko msingi wake.
Kadhalika Mch. Msigwa akizungumzia udhaifu mwingine wa Chadema na vyama pinzani kwa CCM anasema ili vyama viweze kufanikisha shughuli zake na kushinda katika chaguzi ni lazima vijipange kama taasisi na hususan katika ngazi za msingi kama ilivyo kwa Chama Cha Mapinduzi kwani huko ndipo kulipo na ushawishi mkubwa wa wanachama na Vyama hupata fursa ya kushughulikia kikamilifu matakwa ya wananchi kwa ukaribu.
Akikosoa namna ambavyo miundo mingi ya vyama vya siasa ilivyo nchini Tanzania isipokuwa kwa Chama Cha Mapinduzi, Mch. Msigwa anasema upo udhaifu mkubwa kwenye maeneo ya kichama ngazi ya wilaya, Majimbo, Vijiji na mitaa suala ambalo limedhorotesha ukuaji wa demokrasia shindani na hivyo kupelekea Chama Cha Mapinduzi kuonekana zaidi katika ngazi hizo za chini kupita vyama vingine vyote vilivyo na uimara ngazi ya kitaifa peke yake na hivyo kuwalemaza katika kuyafahamu vyema matakwa ya wananchi.