Mchungaji Msigwa: Watanzania tumshukuru Dkt. Nchimbi, 'ametusanua'

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mchungaji Peter Msigwa, aliyedai kwamba hotuba ya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi imewaamsha Watanzania kuwa licha ya kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia ilani yake ya uchaguzi 2025/30 imeweka suala la upatikanaji wa Katiba Mpya kuwa miongoni mwa mambo yake ya msingi katika utekelezaji, lakini wasibweteke kuwa Katiba Mpya itapatikana pasipo kufanya juhudi za makusudi za kupambania

Pia soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Kupitia mahojiano yake na Jambo TV, Mchungaji Msigwa ameibua maswali zaidi ya 10 aliyodai kwamba yanapaswa kuulizwa au kujiuliza kila Mtanzania ikiwemo serikali yenyewe kuhusu utayari, utashi wa kisiasa na nafasi ya serikali katika kuhakikisha hilo linafanyika bila kuhusisha mapambano kama ilivyopendekezwa

Your browser is not able to display this video.
 

Uzuri kwamba kama hawataleta katiba mpya lile azimio la Chadema la No Reforms No Election lipata nguvu zaidi.
 
Huko Facebook Kuna aina ya confession naanza kuiona ikipostiwa na posters kama "watanzania hawanipendi"tena "tutamkumbuka sana samiah"

Sasa najiuliza kauli hizi zinaamaaanisha Nini kama makam nae anakoleza moto kuhusu DAI LA katiba!!?

Tuamini ndio mwisho wa zama za mama au!!?

Maana hata hayati chuma alianza na ngonjera kama hizi!!

Nasubiri kuona!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…