harusi zinafungwa bomani mchana kweupe mtu ana mashahidi wake wawili me na ke, ndoa inafungwa fasta unarudi nyumbani na mke wako mnakula ugali siku inapita, imetoka hiyoWataoana bila kuwaalika ndugu na jamaa mkuu?
Labda ungesema fungu la kumi, ambalo si kila kanisa linalazimisha.Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.
Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.
View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
Baada ya wewe kuchangiwa siyo?Mimi binafsi huwa nachangia misiba, maradhi na dharula zingine za kibinadamu ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka!!!
Nilishaachana na kuchangia harusi miaka zaidi ya kumi iliyopita..... zingine za watu wangu wa karibu.....lakini huo ndo umekuwa msimamo wangu.....
Yaani mi nikuchangie kwenye harusi yako halafu ikifika yangu unajifanya eti ulishaachaga miaka 10 iliyopita this is bull shitMchungaji ale TANO popote pale alipo.
Saivi nina kadi 9 za sherehe ya kupongeza watoto wanaotarajia kugraduu 4m4 na zote ni mwezi huu.
Hivi wakuu katoto kanahitimu tu unaalika na watu kweli?? Tutoe zawadi eti ni ishara ya upendo!!!
Matokeo yanakuja mtoto kapata foo or zero na baadhi kuolewa soon tu baada ya matokeo.
Tupunguzeni kuchangishana kwenye ishuu za kijinga jinga.
Hujanielewa vizuri mkuu. Kama yeye anakataza michango kwanini anapokea michango ya sadaka? Huoni ni double standards mkuu?Labda ungesema fungu la kumi, ambalo si kila kanisa linalazimisha.
Sadaka haina kiwango na sijasikia sehemu wanalazimisha.
Ukimsikiliza vizuri kalalamikia zaidi michango ya harusi kuwa lazima, kalalamikia zaidi michango ya harusi kuwekewa viwango, kaeleza kuwa michango ya harusi inaweka expectations za waliochanga kuchangiwa na wao.Hujanielewa vizuri mkuu. Kama yeye anakataza michango kwanini anapokea michango ya sadaka? Huoni ni double standards mkuu?
Ebu acheni hasira wajinga nyie tunawachangia tunawawezesha kufanya ngono baadae mnaachana mnatujazia watoto mtaani humu tunaanza tena kuombwa hela za shule!Muhuni tu. Hajaoa huyo wala haishi na mwanamke
ushamba gani wakati unapunguza gharama za sherehe?Huoni kuwa kufunga harusi namna hiyo ni ushamba mkuu?
Mimi sikuchangiwa na mtu na ndio maana sitaki kumchangia mtu nje ya mambo niliyoyainishaBaada ya wewe kuchangiwa siyo?
Nilikwisha kujibu hapo awali.Kama anakataza michango ya harusi mbona yeye anapokea michango ya sadaka?
Kwani Yesu Kristo alikuwa na akaunti benki ipi?Anasema kuhusu uchangiaji wa kifedha sio wa kimuujiza mkuu.
TANGAZO
Maimuna maimuna usiniharibie shughuli,,
Jumammosi shughuli ya mwanangu asumani kamaliza la saba
Kama unajua nilikutunza nataka mtunzo wangu,
Sitaki kusiikia umeumwa mama, sjui bibi yako kalazwa mama mtunzo wangu
cc Seran
Lakini anaongea ukweli kuchangia harusi inatakiwa iwe hiyari sio kuvutana mashati na ma card kede kede kama vile mchangiaji ndio muoaji. Harusi inatakiwa maandalizi na iwe haswaa kwa upande wa bwana na bibi harusi ndio wachangiaji. Kuchangia harusi ni utamaduni ulioendekezwa Tanzania na watanzania, mamtoni hamna hizo vitu. Harusi simple, hamna michango wala nini. Mchungaji yupo sawa kabisa.Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.
Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.
View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.