Kuna Mbongo Mnyamwezi wangu mmoja alitoka zake US, karudi Bongo, mchumba wake naye Mbongo katoka US, wamerudi kufunga ndoa na kuishi nyumbani Tanzania.Nawashauri vijana ,wakitaka kuona wajipange kudunduliza FUBA wao wenyewe na wala siwachangishe michango kuwalazimisha watu ,michango iwe ni optional lakini 99% ya gharama zitoke kwa bwanaharusi na bibi harusi.
Yeah! Wabongo wana akili za kipopo sana mkuu. Kuna wengine ukifanya sherehe usiwapelekee kadi watakuua.Kuna Mbongo Mnyamwezi wangu mmoja alitoka zake US, karudi Bongo, mchumba wake naye Mbongo katoka US, wamerudi kufunga ndoa na kuishi nyumbani Tanzania.
Watoto wa Oysterbay long time hawana shida ndogo maisha haya.
Basi Mnyamwezi akawa anawapeleka Wabongo ile Kinyamwezi Nyamwezi mpaka kwenye harusi yake.
Watu wakawa wanataka kumchangia, akawaambia harusi yangu haipokei mchango. Tutafanya kila kitu wenyewe. Ila tuna charity cause huko Umasaini, kuna kijiji kinahitaji maji, kama unataka kuchangia, changia huko kwenye cause yetu kupeleka maji Umasaini kijijini.
Wabongo wengine waliguna sana, wakasema huyu jamaa kukaa Marekani anajiona sana, anaona hataki mchango wa mtu.
Nikasema Wabongo wengine hawana jema, ukiwachangisha lawama, usipowachangisha lawama πππ
Ndio maana nimesema michango ya harusi na sherehe ni suala la kulipana michango ambayo watu wamechangiana. Huyu mchungaji uchwara atuache na shughuli zetu tuhangaike nazo.TANGAZO
Maimuna maimuna usiniharibie shughuli,,
Jumammosi shughuli ya mwanangu asumani kamaliza la saba
Kama unajua nilikutunza nataka mtunzo wangu,
Sitaki kusiikia umeumwa mama, sjui bibi yako kalazwa mama mtunzo wangu
cc Seran
Hakika yaani kwanza unachangiaje wazinifu maana wengi wao walishagatombana...so nikabariki uzinzi wao kwa hela yangu....nopeMimi binafsi huwa nachangia misiba, maradhi na dharula zingine za kibinadamu ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka!!!
Nilishaachana na kuchangia harusi miaka zaidi ya kumi iliyopita..... zingine za watu wangu wa karibu.....lakini huo ndo umekuwa msimamo wangu.....
Sasa chukulia wewe ndiye muoaji. Ndugu na jamaa zako mlialialikwa kwenye kitchen party ya mke wako mtarajiwa mkagida pombe na kula bufee. Halafu wewe unawaambia mimi sitafanya harusi njooni tu kanisani au msikitini mshuhudie kisha mrudi nyumbani kwenu. Hii inakubalika?Ni aibu kufunga ndoa huku unafanya sherehe kwa kutegemea michango ya harusi. Jibebe mwenyewe kisha alika watu waje karamuni. Kama huwezi kujibeba ishia hapohapo unakopaweza. Nenda kanisani/msikitini waone viongozi wa dini wakusajilie ndoa yako kisha rudi nyumbani kale makande yako uliyooandaa, hakuna wa kushangaa, ndio uwezo wako umeishia hapo, usisumbue watu wakupe hela kufanya ufahari na anasa, fanya hayo kwa bajeti yako mwenyewe
mwambieni shayo kwamba wachaga wenzake wanaoongoza kwa kutoa fedha nyingi za michango ya harusiNaingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.
Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.
View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
ebwanaee! Si unajiweza? Fanya harusi kwa bajeti yako, then alika ndugu, jamaa na marafiki zako waje washuhudieSasa watu watashuhudiaje kwamba kweli ulioa na uliangusha harusi babu kubwa? Utasema nini mbele ya jamaa na marafiki pindi wakikuomba mkanda wa harusi waangalie?
Safi ,ndivyo inavyotakiwa hivyo ,tutoe sadaka kwa wenye uhitaji kama msaada na si kwenye harusi na vitu vinavyofanana na hivyo.Kuna Mbongo Mnyamwezi wangu mmoja alitoka zake US, karudi Bongo, mchumba wake naye Mbongo katoka US, wamerudi kufunga ndoa na kuishi nyumbani Tanzania.
Watoto wa Oysterbay long time hawana shida ndogo maisha haya.
Basi Mnyamwezi akawa anawapeleka Wabongo ile Kinyamwezi Nyamwezi mpaka kwenye harusi yake.
Watu wakawa wanataka kumchangia, akawaambia harusi yangu haipokei mchango. Tutafanya kila kitu wenyewe. Ila tuna charity cause huko Umasaini, kuna kijiji kinahitaji maji, kama unataka kuchangia, changia huko kwenye cause yetu kupeleka maji Umasaini kijijini.
Wabongo wengine waliguna sana, wakasema huyu jamaa kukaa Marekani anajiona sana, anaona hataki mchango wa mtu.
Nikasema Wabongo wengine hawana jema, ukiwachangisha lawama, usipowachangisha lawama πππ
Mkuu umemaliza kila kitu. Mfano wa karibu ni kwenye michango ya harusi. Watu wanaifanya kama uwekezaji wa muda mfupi (kugida mipombe na kula mibufee) na muda mrefu (kuchangiwa). Watanzania tumejaa ubinafsi na husda hata kuliko wanyama.Mfumo tuliokuta kwa wenzetu waliotutangalia pengine ndiyo imeathiri mambo mengi
Kwenye upande wa huyo kijana jamii ya kibongo kawaida tuu kuna ubinafsi, na umimi linapokuja suala la maendeleo ya mtu mwingine ikiwa mtu kuomba ada, matibabu, ama kuinuana kiuchumi
Jamii itajenga maswali kwamba huyo mtoto wake nikimsaidia je fadhila zitarud vipi ??
Jamii hiyo hiyo inajenga swali angekuwa mwanangu angesaidiwa ?
Jamii hiyo hiyo itajenga maswali kuhusu tabia za huyo kijana na wazazi hata watangulizi wao ili tuu wapate kushinda wasichangie
Badala yake tumekuta mfumo ya kuwa changia harusi kwa sababu mwanao nae ataoa hivyo jamii itakutenga usipofanya hivyo
ama mtu kafariki mtu anatokea huko ama kikundi na kusimamia kila kitu ilihali walishindwa fanikisha matibabu yake
Hivyo mm nasema kuwa jamii yetu ili ikusaidie inataka kuona msaada huo utarudi vipi kwamba hawatoi kama sadaka ama bure kuna mazingira ya uwekezaji ya kuja kurudisha fadhila waliyokupa