Wang Shu
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 2,562
- 3,715
Inafaa kwa mabachela kama mimi nimejipikia haraka sana bila kuchelewa nikala nikashiba mchana ukapita.
Mahitaji.
Chumvi
Mafuta
Kitunguu kimoja
Samaki wa kukaanga.
Nyanya (idadi uipendayo)
Jinsi ya kupika.
1.Katakata nyanya na vitunguu sehemu tofauti
2.Injika sufuria weka mafuta kiasi yaache yapate moto.
3.Tia vitunguu kaangaa kidogo ikifuatia na nyanya pamoja na chumvi.
4.Funika iache zichemke kwa pamoja dk 10,koroga nyanya zivurugike vizuri tia samaki uache mchuzi uchemke tena upate radha ya samaki.
5.Ipua tayari kwa kuliwa na ugali wako utafurahia mchana wako.
Usisahau na juice mi nilikosa haraka zangu na njaa nikala na ndizi.
Karibuni ya kwisha.