Mchuzi wa mayai!

amu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2012
Posts
16,132
Reaction score
31,149
Leo bwana nimetoka kuzurura nimerudi kulala aaa nikaona kila siku kula kwa jirani noma ngoja leo nikaushe nipike nikaingia rum kuangaza angaza kupika cha dakika 2 akili ikanijia fasta mchuzi wa mayai bahati nikawa na mayai akiba ndani,nyanya,vitungu yaani mazagazaga yote full.ngoja nishare na nyie msosi simple mzuri ndani ya dakika kumi umeshamaliza.

Jinsi ya kuandaa [inategemea na idadi mie nlikuwa napika cha peke yangu]

-niliwasha kajiko changu cha mchina

-chemsha mayai mawili,

-wakati yanachemka nikakata kitunguu maji kilikuwa kikubwa nikatumia nusu,

-nikasaga nyanya 3 kwenye ile blender ya mkono/carot machine

-nikamenya carrot kidogo na kuikatakata slices ndogo ndogo,

-nikatwanga vitunguu swaumu kiduchu.

-Mayai yakaiva nikayaipua na kuyaweka kwenye sahani nikabandika

-sufuria nikadondoshea mafuta ya kupikia kidogo,

-nikaweka vitunguu na karot nikaanga mpaka vitunguu rangi ya brown kisha nikaweka nyanya na vitunguu swaumu nikafunikia,

wakati vinachemka nikawa namenya/kutoa maganda mayai yangu 2 ,

-nyanya zikaiva nikadondoshea curry powder kiduchu,

-kisha nikadondoshea nyanya ya pakti kidogo,

nikafunikia tena,

-baada ya dakika 1 nikakatia katia hoho kiduchu nikaweka na limao nusu kipande nikasubiria hoho zikaiva kisha nikaweka mayai nliyoyamenya nikaacha vichemke kama dakika 2 kisha nikaipua.

Ndani nlikuwa na mkate nikala zangu na mkate na chai ya rangi hapa nimeshiba top na yai moja na mchuzi wake limebakia nitanywea asubuhi.

Hii mboga nzuri hata ukiwa na family unaweza ukalia na wali au spagheti[mie mara ya kwanza nilipanga kupika na spagheti but njaa iliuma sana ha ha pia kubana mafuta ya taa bajeti loo.
bak ladyfurahia mimisa me370 kipaji halisi mentor single boys hii inawahusu sana looo paloma mwaj shansarie kiwatengu gfsonwin snowhite smile kongosho badili tabia king'asti munkari lady doctor mr rocky filipo arushaone munkari monaco mwita maranya faizafoxy heaven on earth simplicty lara 1 kokutona ynnah mwanyasi watu8 charminglady husninyo mamndenyi vin diesel bujibuji preta marejesho arabella dark city yule kaka anayependa misosi nani vile aaaa nshamkumbuka ritz
 
wanajf chef woteee jaribuni hii kupika kwanza haina gharama na chakula cha chap chap uwiii Kaizer ilikuwaje nikakusahau jamani? Uje na wakezo wote AshaDii DEMBA na wengine
 
Last edited by a moderator:
duh mimi nimechemsha mayai mawili basi...what a coincidence amu?...huu ubachelor huu.
ila mi napenda mchuzi wa mayai sema mie huwa sichemshi kwanza
nakaanga vitunguu ..nyanya karoti hoho ...vikishaiva then namwaga mayai ni mboga nzuri sana hata kwa ugali
 
amu familia yangu kuuubwa nikipika ya hivyo lazima ninunue tray zima.

Though nishawahi kuila kwa rafiki yangu, iko powa.
DEMBA hakikisha kaka swahiba Kaizer anapata hii menu


Wanchekesha Koku......


Ahsante kwa kitchen lesson amu. Ngoja kesho my wife wangu Lady doctor anipikie kwenye breakfast hayo makitu.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha umenikumbusha mbali sana aisee, ngoja paw asome hii hapa.
Unaweza pia usichemshe mayai. Unayapiga tu na chumvi. Ukishafikia nyanya na vizagazaga vimeiva uanmiminia mayai na kukoroga kwa bidii hadi yagande. Unapata bonge la mboga. Hiyo unaweza weka katikati ya mkate wako. Mimi sio mpenzi wa michuzi, so ile ya mayai ya kuchemsha naiepuka.

Lets get proffessional, living a 5* life. Ukishamenya mayai yako unaweza kulikata kati fyaaap. Inapendeza kweli kile kiini kikionekana
 
Hahaha umenikumbusha mbali sana aisee, ngoja paw asome hii hapa.
Unaweza pia usichemshe mayai. Unayapiga tu na chumvi. Ukishafikia nyanya na vizagazaga vimeiva uanmiminia mayai na kukoroga kwa bidii hadi yagande. Unapata bonge la mboga. Hiyo unaweza weka katikati ya mkate wako. Mimi sio mpenzi wa michuzi, so ile ya mayai ya kuchemsha naiepuka.

Lets get proffessional, living a 5* life. Ukishamenya mayai yako unaweza kulikata kati fyaaap kabla ya kuweka mchuzini. Inapendeza kweli kile kiini kikionekana.
 
Kumbe ni mapishi kweli??

Nilidhani ni yale mambo yetu ya Makorora kwenye kijiwe cha thupu ya pweza....

Nilikuwepo kiduchu...lol!!


Babu DC!!
 
Mboga ya kibachela hii lakini ni tamu sana hukawii kunogewa na kuchonga mzinga ukiwa unaikumbuka kumbuka kila baada ya muda ukaitamani tena.
 
wanajf chef woteee jaribuni hii kupika kwanza haina gharama na chakula cha chap chap uwiii Kaizer ilikuwaje nikakusahau jamani? Uje na wakezo wote AshaDii DEMBA na wengine
amu naona njaa na si ajabu hata jikon ulisahau kuzima kisa unasingizia njaa
 
Last edited by a moderator:
haa haa haaaa haaaa ntasahau vipi besti. bila hiyo makitu unafikiri angewasahau wale wake wenzangu?

heeee baby DEMBA sijawasahau hata chembe....ungependa niwasaua jamani?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…