Mchuzi wa vibua (samaki wadogo)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mchuzi huu hufaa wale wenye familia kubwa,
Mahitaji:
fungu moja la vibua,
vitunguu,
nyanya,
tomato paste,
limao,
chumvi, oxo.

Osha vibua toa utumbo na vichwa,
Weka limao na chumvi,
Chemsha kwa dakika kumi toa na uwache wapoe.

Wakipoa toa ule mwiba wa katikati na miba mingine ukiweza. Chambua minofu Ile ya samaki iwe kama nyama ya kusaga.

Kaanga kitunguu mpaka kiwe hudhurungi,
Kata nyanya vipande vidogo kaanga pamoja na vitunguu,
Ongezea pilipili (kama ni mpenzi),
Weka tomato paste, na minofu ya vibua, chumvi na limao, acha ichemke kwa moto mdogo kwa nusu saa.

Mchuzi huu huliwa na ugali au ugali wa muhogo.
 
Kapicha ka vibua mkuu
 
Huyo samaki alisha nishindaga kitambo sana kutokana na shombo lake
 
[emoji3][emoji3][emoji3] aaahaa haaa haaaa...Mr.Mtui iko kitu umenikumbusha nimecheka saana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mtuiiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…