MCL, ATOGS, TZLPGA zatia saini kuandaa Kongamanano 'Energy Connect 2024

MCL, ATOGS, TZLPGA zatia saini kuandaa Kongamanano 'Energy Connect 2024

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Muhtasari. Kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo "Ushirikiano wa Kibunifu katika Nishati safi ya kupikia, Endelevu na mustakabali wa Kijani," litafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 16 hadi 18 2024.

Sute Kamwelwe na Aurea Simtowe

Dar es Salaam. Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Gesi za Mitungi Tanzania (TZLPGA), kwa pamoja wametia saini Mkataba wa Makubaliano kuandaa Kongamanano la Nishati Safi liitwalo 'Energy Connect 2024'.

Kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo "Ushirikiano wa kibunifu katika Nishati safi ya kupikia, Endelevu na mustakabali wa Kijani," litafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 16 hadi 18 2024.

Lengo kuu la Kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wadau mbalimbali ndani ya sekta ya Nishati na mashirika na kampuni katika sekta zingine zinazo tambua thamani wa nishati safi kwa jamii.

Akizungumza baada ya utiaji saini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Victor Mushi amesema matumizi ya mkaa na kuni yanaathari kiafya hivyo wameona waungane na Serikali na wadau kuwakwamua watu wanaotumia nishati hizo wahamie katika nishati safi za kupikia.

"Tumejizatiti kwenye kuongeza uhamasishaji na kutoa uelewa mkubwa kwa jamii nchini nishati safi ya kupikia, kupitia majadiliano na kuleta suluhisho za kibunifu ambazo zitatokea katika tukio hili.

"MCL tutashirikiana na Serikali Pamoja na sekta binafsi na sizo binafsi kwenye kuelimisha jamii kwa njia bunifu kuhusu utumiaji wa Nishati safi na salama kwa mazingira na Afya," amesema Mushi.

Amesema Kongamano la Energy Connect 2024 ni uthibitisho wa kujitolea katika kuunga mkono vumbuzi endelevu na jitihada zinazofanywa mpaka sasa na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa sera ya Nchi, katika kufanikisha malengo ya nishati safi ya Tanzania.

Kwa upande wake Abdusamad Abdulrahim, Mwenyekiti wa ATOGS, amesema dhumuni la Kongamano ni kumtua mama kuni ambazo zinaathari kwa afya ikiwemo kupofua macho.

Amesema muunganiko huo ni kuleta nguvu pamoja kwani kidole kimoja hakivunji chawa. Pamoja na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutaka asilimia 80 ya Watanzania watumie nishati safi hadi ifikapo 2034.

"Aidha, tukio hili litakutanisha wadau muhimu kutoka kwenye mayororo wa thamani wa nishati ili kuchunguza suluhu za ubunifu zitakazounda mustakabali wa Tanzania.

" Tunaamini kuwa kwa pamoja, tunaweza kufanya maendeleo makubwa kuelekea kufanikisha mustakabali wa nishati endelevu kwa Tanzania"

Amesema Kipaumbele ni teknolojia na nishati safi kila kona ya Tanzania watu wapewe vitendea kazi na teknolojia waweze kukacha matumizi ya kuni na mkaa.

"Wito wangu kwa Watanzania kwanza lazima tuimbe wimbo mmoja lazima twende kwa pamoja hadu waliopo vijijini tushiriki kwa siku hizi tatu ili tukomboe Watanzania wanaotumia kuni na mkaa," amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Gesi za Mtungi, Mhandisi Amos Jackson, amesema Kongamano hilo ni sehemu ya kutoa elimu na kuishirikisha na Serikali katika changamoto zilizopo.

Amesema LPG inamchango mkubwa huku lengo la Serikali kuwataka Watanzania watumie nishati safi ya kupikia litawezekana kupitia nishati hiyo.
 
Back
Top Bottom