MDA & LGA's

ekam master

Member
Joined
Aug 17, 2024
Posts
46
Reaction score
55
Wakuu samahani naomba kujuzwa kuhusu ajira zinazotangazwa na MDA & LGAs. Hapa kwenye 'MDA' mara nyingi naona hizi taasisi zinazojitegemea zinatangaza nafasi za kazi zenyewe mfano TRA, TANAPA, TAKUKURU nk, sasa je hizi zinazotangazwa kupitia MDA & LGAs waajiriwa wake hupelekwa katika taasisi gani ikiwa hizi taasisi bado zinaajiri zenyewe? Au kuna taasisi ambazo haziruhusiwi kujiendeshea mchakato wa ajira!
 
min -me akija anaweza akakuuliza tahasisi ni nini na waajiliwa ni nini? 😅😅😅.

Anyway, ngoja waje watupe muongozo mkuu.
 
min -me akija anaweza akakuuliza tahasisi ni nini na waajiliwa ni nini? 😅😅😅.

Anyway, ngoja waje watupe muongozo mkuu.
Haha sawasawa mkuu. Kwenye taasisi hapo nililenga tu [independent departments, na agencies] mara nyingi naona zinajitangazia posts zenyewe. Tafsiri yake hizi zinazotangaza zenyewe hazina habari na posts za MDA.
 
Haha sawasawa mkuu. Kwenye tahasisi hapo nililenga tu [independent departments, na agencies] mara nyingi naona zinajitangazia posts zenyewe. Tafsiri yake hizi zinazotangaza zenyewe hazina habari na posts za MDA.
Unataka ajira TRA alafu hauwezi kutofautisha kati ya Taasisi na Tahasisi.
 
Mkuu kwa ninavofahamu kwa sikuhizi.. izo taasisi zina njia mbili za kuajiri, either ziajiri zenyewe kama taasisi au ziajiri kwa MDA & LGA kupitia utumishi, na sehemu wanapopelekwa ni sehemu izoizo (ikiwa taasisi itashindwa kujiendesha yenyewe kufanya mchakato wa ajira, itaomba watu kutoka uko mda&lga.. Kwaio ukiomba mda&lga unaweza kuta umetupwa popote ambapo pana uhitaji wa watu wa io fani yako.
 
Karibu Halmashauri mkuu tupambane
 
Karibu Halmashauri mkuu tupam

Asante, nashukuru sana, nimekuelewa vyema.
 
Asante, nashukuru sana kwa ufafanuzi wako. Shukuran sana.
 
Ukiona taasisi imetangaza yenyewe nafasi za kazi fahamu kwamba watumishi walipangiwa kazi katika taasisi hzo kupitia Sekretarieti ya ajira walikuwa mabomu kuliko taasisi ilivyotegemea. Kwa mfano waajiriwa wengi waliopelekwa TRA kupitia sekretarieti ya ajira wamegeuka mizigo kuliko ilivyo tegemewa. Sasa mtu anaenda kumkadilia mfanya biashara kwenye interview unamuuliza mapendekezo ya kamati ya jaji Hosoro na professa Mluma?
 
Kwa sababu ambazo hazipingiki ni dhahiri taasisi zinazoweza kukinga kifua kwamba zinataka kuajiri zenyewe ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee. Kwa sababu ya unyeti wa masuala yao. Aidha, taasisi nyingi zilizobaki usaili wa kupata watumishi wapya unaweza kusimamiwa na Sekretariet ya Ajira na wakapatikana watumishi wazuri tuu! Vinginevyo, kutakuwa na ukakasi tuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…