Mdada na chabo !

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
Hii nimekumbana nayo jana pale mtaani kwetu. wakati tukiwa tunasubiri kuangalia mechi ya Man Utd na AC Milan, ghafla nilistushwa na zogo nje ya nyumba ninayoishi. Nilipotoka kujua kulikoni nilishangazwa na nilichokuta. Binti wa kama miaka 23 hivi na namfahamu kwani huwa namuona hapo mtaani, amekunjwa gauni lake na mama mmoja kisa eti alikuwa anawachungulia huyo mama na Mr. wake wakiwa kwenye malovee yao kwa kweli alimkwangua makofi ya hatari... Najua kupiga chabo si jambo geni ingawa kwa ufahamu wangu mara nyingi hufanywa na wanaume/wavulana. Sasa huyu ni binti...Hii imeakaaje jamani...
 
pengine ni kidumu cha mdingi hivo alipojua leo yuko kwa bi mkubwa akataka akaone ili ikiwa zamu yake ajue amteke vipi,
mh kweli kaaaaaaazi ipo.
 
Umesahau kuandika namba ya simu yake huyo, anahitaji msaada wa haraka sana.
..Nahisi mayanki wa mtaani pale watam-keep busy sana baada ya lile tukio maana wengi wamejitolea kumsaidia huenda akapunguza kama sio kuacha kabisa kupiga chabo..
 

Ohh, kweli bado hujaiona dunia..he he he..Kuna wanawake wanafuga 'nyoka' katikati ya miguu yao..lol
 

Mmh wakati tuko chuo kulikuwa na mdada mmoja alikuwa mtaalamu wa kula chabo. Alikuwa anakaa summit ya hall four na washkaji wanakula chabo.

Madai yake ilikuwa inampandisha mzuka kwa ajili ya kumservice boyfiend wake. To her it was a hobby in the same category kama wanaume.

Mi kama mwanamke nilikuwa namshangaa but i guess kila mtu ana namna yake ya kupandisha steam. Wengine wanaangalia X na wengine wetu glass ya wine tu mzuka debe.
 
Nimeipenda sana hii kwani imetulia sana, naam ni nzuri kwani si tunadai haki sawa kwa wote. Pia si kila anachofanya mwanaume mwanamke anaweza sasa tatizo ni nini?
 
Maskini pole yake kwa kupigwa!
utoto unamsumbua akikua ataacha
 

Kumbe na wewe una mbwembwe!!
 
Maskini pole yake kwa kupigwa!
utoto unamsumbua akikua ataacha
...Miaka 23 nawe wamwita mtoto!! Kwa umri wake anapaswa kupiga kura awamu mbili, aweza kuolewa, aweza kila kitu!!
 
Mzee usimcheleweshe kabla mihemko haijamlala. Mtafute umwepushe na nadharia za ngono. Atakushukuru
 
du nilizani wapiga chabo ni kina kaka tu,kumbe na wamama hatuko nyumo!lol
 
du nilizani wapiga chabo ni kina kaka tu,kumbe na wamama hatuko nyumo!lol
...Usipime! sijui inakuwaje hii mi mwenyewe iliniacha hoi...lakini nadhani binti alikuwa ana-enjoy sana chabo maana kwa maelezo ya yule mama alishamstukia zaidi ya mara 3 huko nyuma ingawa hakumtonya mzee wake. Sasa mpaka amekutwa eneo la tukio huenda ganzi ilifika mahali pake akashindwa hata kukimbia....
 
Duu mambo ya uswazi hayo..Au kanatembea na mume wa huyo mama sasa mawivu yalimshika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…