Very shallow!
Kwa taarifa yako wengi wetu hapa tunapigania ukombozi wa kweli... Ukinichukua leo nikapige kura kuna wagombea wawili ambao ni Dr. John P Magufuli (CCM) na mwingine yeyote isipokuwa Dr Slaa wa Chadema nitampigia Dr Magufuli kwa sababu ninaheshimu mchango wake na wala si chama anachotoka
Kwenye mdahalo wa wagombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini uliorushwa na kituo cha TBC1 jana usiku,mgombea ubunge wa NCCR-Mageuzi kwa kiasi kikubwa alimfunika yule gabachori wa Chadema.
Wadau mliupimaje ule mdahalo?
Very shallow!
Kwa taarifa yako wengi wetu hapa tunapigania ukombozi wa kweli... Ukinichukua leo nikapige kura kuna wagombea wawili ambao ni Dr. John P Magufuli (CCM) na mwingine yeyote isipokuwa Dr Slaa wa Chadema nitampigia Dr Magufuli kwa sababu ninaheshimu mchango wake na wala si chama anachotoka
hata akishinda wa Nccr Mageuzi poa, akiwa wa DP ni poa, kwangu ili nchi ikombolewe ni lazima kuwe na mageuzi/mabadiliko. kisha mambo mengine yatakuja.
nchi hii hatuheshimiani kwakuwa kuna genge la watu linalojiona limeumbwa kutawala, hili genge liko ccm.
tunahitaji mabadiliko kwanza , kisha mengine Tutazidishiwa.
yule bwana wa chadema hana takwimu kabisa kwa kitu ukilinganisha na wa nccr ambaye alikuwa akijibu kwa takwimu.
najua hoja hii si nzuri kwenu,na wengi mliangalia,mnafahamu nini kinaongelewa.
ni kweli,hapa ni kumsifia mtu yeyote wa chadema hata kama amevurunda.
Mgombea wa Chadema jimbo la Kigoma Kusini oyee!
Ndo maana Zitto alisema kuwa atamuunga mkono kijana huyu hata kama hayuko Chadema.
Bwana nilicheki ule mchakato mmh ama kweli vijana waongea. Walikua jamaa wawili mmoja wa CHADEMA na Mwingine wa NCCR, all these guys were very competent. Walikuwa vizuri sana and they were very young.
Kingine kilicho nishangaza huko Kigoma kusini ni jinsi wananchi wa kule walivyokuwa na constructive questions. Wale jamaa sijui wamesoma wapi maanake walikuwa wanahit points kwenye maswali yao. Kila aliyeuliza swali awe mzee ama kijana aliuliza swali la msing. Mfano kuna mzee mmoja aliuliza swali kuhusu uhaba wa elimu ya uraia jimboni mwao.
Generally i was so impressed with those guys.
Uko sahihi, yule bwana analijua jimbo analotaka kugombea kwa kila hali, jiografia, uchumi, miundombinu etc. Anajua matatizo yao anajua anataka kwenda bungeni kufanya nini.
Ningekuwa Kigoma kusini Ningempa kura yangu, tunahitaji wabunge wengi wa namna ile baada ya mika mitatu atakuwa Zitto Kabwe mwingine.
Ni hazina kubwa.