Elections 2010 Mdahalo WA JK: WANA CCM TUSAIDIENI KUULIZA MASWALI HAYA


HEHEHEHE! AHSANTE!
:smile-big:
 
Bajeti ya ziara za raisi nje ya nchi ni shilingi ngapi na katika hizo ametumia kiasi gani kwa miaka hii mitano iliyokuwa madarakani......???

Nadhani swali lako ni la muhimu sana. AU tunaweza kuuliza Je fedha zilizopatikana kutona na safari zako zinafikia kiasi gani? Na je safari hizo ziligharimu kiasi gani? Kwani unaweza kuta ni lile la watu fulani wanauza ng'ombe kwa kesi ya kuku.
 
Naomba muongeze maswali kwani ni vizuri ukaona ni kwa nini CCM haikutaka mdahalo unaweza kutokeza maswali haya.
Kuna swali nimesahau.
Kinana alisema Chama chake kinafahamika hivyo wamegundua kuwa wapinzania wanataka kujulikana kwa kupitia mdahalo. Swali Je CCm imesahaulika hadi wameona wafanye mdahalo usiokuwa na wapinzani? Je kushiriki kwa Kikwete kipindi hiki haonii kinaenda kinyume na utaratibu wa CCM kupitia katibu wake mkuu kuwa MDAHALO NI MARUFUKU?
 

Kwa maana halisi ya ustawi wa taifa hayo madudu uliyoandika hapo hayana nafasi kabisa
 

Mbona naona kama uko nje ya mada, naona kama umukurupuka! Nakushauri usome tena kichwa cha habari.
 
Wapinzani wanasema Watahakikisha Rasilimali za Taifa zitatumika kwa manufaa ya Watanzania, Wewe hujaliongelea hili kwenye mikutano yako. wewe una mtazamo gani kuhusu hili?
 

UDINI?
Unajua dini za wagombea wa CCM?
Rais, makamu, rais znz?

Pili akili huna, unadharau elimu ya biblia? Ndugu, ukisoma biblia, huna hata haja ya kwenda darasani saaana, kwani hata baiolojia imo humo ndani. Hivi uliambiwa kuwa kuna shule ya urais? Kwa haya mawazo yako, hata shule ya awali hukwenda. na kama ulienda, una umaskini wa kufikiri. Pole sana.

Uliongea na huyo mwanamke akakwambia ni mke wa mtu? usiropoke tu, humu ni sehemu ya great thinkers, nenda blog ya JK uweke mambo hayo siyo huku. Humu watu wanatafakari hoja mzee, pole na upuuzi wako huu.
 
Mimi naomba mumuulize rais wetu kama ni kweli aliahidi bajaj 400 za kubeba wajawazito. Na kama ni kweli naomba wamuulize rais wetu anayetupenda atuambie Tz ina wilaya na vijiji vingapi na zitapata bajaj ngapi na hizo bajaji zitapita barabara zipi huko vijijini. Mwisho wamuulize rais wetu, atuambie serekali yetu ina mashangingi mangapi na kwa nini asichukue japo robo tu ya hayo mashangingi akayajeuza ambulance badala ya kufanya ambulance bajaj?
 
lazima utakuwa hujaelewa nini muanzisha hii mada anataka..........!!!!
ni kweli tunajadili mambo ya maana yeye analeta ujinga wake hapa, slaa anaingiaje hapa sasa! Mbona watu wapuuuzi ndo hawa jk anawaita majuha!
 
We BULL acha ukereketwa, weka ushabiki mbali toa majibu kwanza ya CCM then tutakuja kumjadili DK Slaa. Tuwe fair tuanze upande wa CCM kwanza.
 
Naomba wamuulize kuhusu safari zake za nje akiwa raisi ataendeleza????
 
Watauliza live wale watakaoingia katika mdahalo. Utaenda?
Kwa uelewa wangu mdahalo ni pale ambapo watu wawili au zaidi wanaendesha mjadala na kugunganisha maoni na mitazamo. Unapokuwa peke yako unaulizwa maswali na kujibu huo siyo mdahalo. Labda tuite mahojiano.
 
1. Je ni mambo gani yamekukwamisha kutimiza nyigi ya ahadi unazotoa ktk kipindi cha miaka mitano iliyopita?

2. Ukifaulu kupata uraisi utaenda lini kwa obama?
 
Nilitamani tungeuliza haya. Je unadhani haya yaliyo hapa yamejibiwa? Kama la basi toa uamuzi wa busara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…