Usiku wa kuamkia leo Jumatano Septemba 11, 2024 wagombea urais wa Marekani, Donald Trump (Republican) na Kamala Harris (Democratic) wamefanya mdahalo wa kutoa hoja zao mbele ya wananchi huku wakinyukana kwa hoja.
Mdahalo huo ulioandaliwa na kituo cha luninga cha ABC, mbali na hoja za wagombea hao, pia ulitawaliwa na kushutumiana kwa mambo mbalimbali ikiwamo ukosefu wa ajira na sera mbaya za mambo ya nje.
Wakifunga mjadala huo, Kamala alichagiza kuwa “Tumesikia maono mawili kwa nchi yetu yakiwamo yatakayoturudisha nyuma na maono mengine ambayo yatatupeleka mbele (akijipigia chapuo).”
Kwa upande wake, Trump akimjibu kuhusu hilo alisema: “Hatuwezi kutoa sadaka nchi yetu kwa ajili ya maono mabaya. Tumeachwa nje duniani kote.”