Mdahalo wa urais Marekani Trump, kamala wanyukana wakishutumiana

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Usiku wa kuamkia leo Jumatano Septemba 11, 2024 wagombea urais wa Marekani, Donald Trump (Republican) na Kamala Harris (Democratic) wamefanya mdahalo wa kutoa hoja zao mbele ya wananchi huku wakinyukana kwa hoja.

Mdahalo huo ulioandaliwa na kituo cha luninga cha ABC, mbali na hoja za wagombea hao, pia ulitawaliwa na kushutumiana kwa mambo mbalimbali ikiwamo ukosefu wa ajira na sera mbaya za mambo ya nje.

Wakifunga mjadala huo, Kamala alichagiza kuwa “Tumesikia maono mawili kwa nchi yetu yakiwamo yatakayoturudisha nyuma na maono mengine ambayo yatatupeleka mbele (akijipigia chapuo).”

Kwa upande wake, Trump akimjibu kuhusu hilo alisema: “Hatuwezi kutoa sadaka nchi yetu kwa ajili ya maono mabaya. Tumeachwa nje duniani kote.”

 
Usiku wa kuamkia leo jumatano 11 september 2024 , wagombea urais nchini Marekani Donald Trump (Republican) na Kamala Harris (Democratic)wamefanya mdahalo na kutoa hoja zao mbele ya wananchi huku wakinyukana vikali kwa hoja, mbali na hoja zao mdahalo huo ulitawaliwa na kushutumiana baina ya wagombea hao wawili katika masuala mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira na sera mbaya za mambo ya nje.

Wakifunga mjadala huo kwa Kamala kuchagiza kuwa "tumesikia maono mawili kwa nchi yetu yakiwermo yatakayoturudisha nyuma na yatakayotupeleka mbele." Kwa upande wake Trump aimjibu" Hatuwezi kutoa sadaka taifa letu kwa maono mabaya .tumeachwa nje ya dunia kote."

 
Nahisi kama kuna rafu ilifanyika kwa Trump, inawezekana kamala alipewa maswali kabla, Sikutegemea ile performance ya Kamala, ila sidhani kama ana nafasi kubwa ya kushinda
 
Japokuwa Nina mashaka juu ya kushinda kwa Kamala Harris, lakini ukweli mchungu sana unabaki kuwa Trump Siyo mtu sahihi wa kuwa tena Rais wa Marekani.
 
Tungeweza na sister kufanya midahalo kamawenzetu,ingekuwa safi nakumbuka 1995 Mdahalo kati ya Mrema,Lipumba na Mkapa ndio tuliweza kubaini uwezo wa Mkapa na Lipumba,lakini huu mtindo wa kuletewa wagombea watueleze tu wanayotaka was so poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…