Elections 2010 Mdahalo wa wagombea ubunge vijana....ccm kama kawaida wameingia mitini!

Elections 2010 Mdahalo wa wagombea ubunge vijana....ccm kama kawaida wameingia mitini!

BornTown

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2008
Posts
1,716
Reaction score
482
Wanajamvi juzi jumamosi kulikuwa na Mdahalo LIVE kupitia ITV uliokuwa uanafanyika MovenPick Hotel chini ya mwenyekiti Jenerali Ulimwengu.

Mdahalo ulikuwa kuwakutanisha wagombea Ubunge Vijana watueleze sisi wananchi kwanini wagombea na ulikuwa ni wa vyama 3: CCM,CHADEMA na CUF. Kama kawaida CCM walipotea hawakuonena ingawa kulikuwapo na makada wa CCM ukumbini.

Mdahalo ulikuwa mzuri kwani maswali yaliokuwa wakiulizwa yalikuwa ni mazuri, walizungumzia mambo ya ELIMU,AFYA,AJIRA na UFISADI

Swali: 1. JE CCM HAINA WAGOMBEA VIJANA???
2. NA KWANINI WALIKUBALI KUSHIRIKI HALAFU WAKATOKOMEA KUSIKOJULIKANA?
3. HAO MAKADA WALIOKUWAPO UKUMBINI WALIKUJA KUFANYANINI AMA
WALITUMWA NA NANI?
 
Back
Top Bottom