Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.

Shalom

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2007
Posts
1,315
Reaction score
125
:crying:Wapendwa,

Kwa TZS 100,000 watu 100 JF tunaweza kuandaa mdahalo wa urais.

Muda wa kupiga domo umekwisha je? Tunataka na mwaka huu kusiwe na mdahalo kama 2010? Je unadhani kuna mtu mwingine wa kuanzisha hili swala zaidi ya JF? Mimi nadhani haiwezekani. Basi kama unaona hili jambo ni zuri na uaweza support basi orodhesha jina lako hapa ili tuwape moyo viongozi wetu wa huu mtandao waweze kufanya mambo makubwa. Kama kuna chama hakitashiriki basi ni kivyao vyao

Tafadhari siitaji matusi na kejeli ukiona hili wazo halifai nenda kwenye topic zingine.

1. Shalom TZS 200,000 (ameshatoa 100,000!)
2. Nyani Ngabu $500 (TZS 750,000)
3. Invisible TZS 300,000/=
4. De Novo TZS 200,000/=
5. Lusajo L.M TZS 50,000/=
6. Mchukia Fisadi TZS 50,000/=
7. Mtu wa Pwani TZS 1,000,000/=
8. Chakaza TZS 100,000/=
9. Ntemi Kazwile 50,000/=
10. Natasha Ismail 50,000
11. MC 50,000 (Ametoa yote!)
12. Nyambala ($100) 150,000
13. Selous 50,000
14. Kisoda2 50,000 (Ametoa yote!)
15. Chesty 50,000
16. Ndege ya Uchumi 50,000
17. Mzee Mwanakijiji (atatoa ahadi)
18. Misonge 50,000
19 Mtwa 200,000
20. Steve Dii 80,000
21. Acid 200,000
22. Masanilo a.k.a Shalom au Mzee wa Texas 50,000

Jumla ya ahadi so far ni TZS 3,730,000. Cash so far 200,000 Thanks wazalendo kwa kuwa tayari kutengeneza historia!
 
Nitachangia TZS 300,000/=

Wasiwasi wangu ni kama JK atakubali. Kama itawezekana basi tunaweza kulifanikisha hili
 
Nitachangia TZS 300,000/=

Wasiwasi wangu ni kama JK atakubali. Kama itawezekana basi tunaweza kulifanikisha hili

Yeye tunamjua sana kuliko hao wangombea wengine kwa hiyo itakula kwake tutakapo wajua wengine kama yeye
 
Mimi naahidi laki mbili... na kama ikibidi tufikishe saini 1000 na kila saini tuidhamini kwa elfu kumi tu!!!
 
Je mnaonaje pia pakawa na focus ya maswali kabisa kwenye kila area muhimu kwa maendeleo ya nchi na hata maswali tukayaweka humu na hawa candiates wakajiandaa nayo?
 
Je mnaonaje pia pakawa na focus ya maswali kabisa kwenye kila area muhimu kwa maendeleo ya nchi na hata maswali tukayaweka humu na hawa candiates wakajiandaa nayo?

Hapana, wasipewe maswali maana wataenda kukariri majibu. Sisi tunataka kujua off the top of their heads kama kweli wanajua issues. Wanachoweza kupewa ni focus areas...kwa mfano, sera ya mambo nje, mambo ya ndani (with uchumi being the main concentration), elimu, ulinzi, n.k. Maswali mahsusi wasipewe. Labda kama nyinyi mnataka kusikia majibu yaliyokaririwa lakini mimi sitaki hayo.
 
noted with thanks

kwa staili hiyo wataingia mitini mazee
 
Hili ni wazo jema sana na ilinisikitisha sana pale 2005 ilipopita bila ya kuwa na Mdahalo. Na kama tutaandaa itawa ni vema sana kukawa na muongozo wa maswali na kinachoweza fanyika ni kuwajulisha tu wahusika kwamba mdahalo utagusia maeneo kadhaa wa kadhaa.

Kila mtu hujikuna pale ambapo mkono wake unafikia. Kwa upande wangu nahaidi kuchangia TZS 50,000 katika hili.

Ahsante.
 
Hili wazo ni zuri sana sana, ila mbona kama kunakukanyagana miguu? nimeona watu wanaitwa Vox media wameshaanza na waliokua wagombea Zanzibar na wanampango wa kuendelea na mjadala huo, STAR TV nadhani wamewapa sponsorship ya air time sasa hii iniative itakua na utofauti gani na hiyo iliyokwisha anza? mi nadhani JF waendelee na hii monitoring na promotion ya strategy kuliko kutaka kuanza na kitu kipya kabisa. Halafu siji hizo hela zinazochangwa ni kwa ajili ya nini maana hawa wahojiwa wa level hiyo hawahitaji kulipwa na pia any TV station ukiiendea na deal kubwa kama hiyo na kuwahakikishia umeshampata watakukimbilia tu.kwa nini usijadili na hao vox kuona kama mnaweza kuongeza nguvu? contact ni Ansbert Ngurumo deputy editor wa Tanzania daima.
 
Tunahitaji midahalo kama mitatu hivi, hao vox kama wameanza basi ni vizuri lakini ukimtegemea mwenzako pindi akighairi unakuwa huna alternative. Tunachoweza kujadiriana na hao vox ni pengine kugawana theme. TUnahitaji kuchanga ili tuweze kuwa na jeuri ukitegemea cha bure wenye TV wakikataa ukiwa na hela hata Citizen ya Kenya wanaweza kurusha! Hata ,ukipata ya bure bado kuna matangazo na other preparation

Asante kwa mawazo yako na sio lazima kila mtu achangie si unaona kuwa watu chache sana wamereply hapa? nenda kaangalie topic za mipasho utakavyoona wengi, we need real people here
 
Mmh!, sasa tunaelekea kuzuri. Kama hili wazo likifanikiwa litakuwa jambo jema sana. Nami naahidi kitu ila nitasema baadaye ni kiasi gani.
 
ms atatoa 1 m ili kufanikisha mdahalo, lkn kwanza tumngoje mgombea wa chadema kama hatakuwepo sitoi

Thanks, Lakini natia shaka kama mtu mwenye IQ yako anaweza ku rise 1M anyway unaweza kuwa exceptional na watu wa level yako. thanks any way!
 
Mi nitachangia 50,000 ya kitanzania.
Ila najua Kikwete na sisi m yake hawatakubali maana amezoea kuwasomea zile rubbish kaandikiwa na January na kuwasomea vichwa wazi na hawaulizi maswali.
Kama nasema uongo mwambieni ahudhurie huo mdahalo kama atakubali.
 
Mbezi (Morogoro road)-Malambamawili-Kinyerezi-Banana (Km
14.0);

barabara hii tayari iko kwenye ujenzi au hatua zaq mwisho kukamilika sasa sijui hii ilikuwa ilani ya 2005-2010 au 2010-2015 nilitegemea waweke kitu kingine hapa
 
Du kazi kweli kweli!

Jamani hima basi! hata Book tano kweli zinatushinda?
 
naomba mtu aniambie mdahalo huu utafanyika live on TV??
kama jibu ni ndio,je utafikia % ya wapiga kura??
je huu MDAHALO utaweza vipi kubadili mentality au kuwaelimisha wale 70% ambao naamini hawana access ya mtandao au hata tv.....
mdahalo huu ni muhimu kama wapiga kura wengi wangekuwa na akili/mawazo ya wana-JF,otherwise mdahalo huu hautasaidia chochote,inabidi itafutwe njia nyingine ya kuelimisha wapiga kura.......wale 70% ambao wengi wako hukooooo ambako hakuna hata umeme......
 
mimi niko tayari kutoa 1000000 ila kuwe na mdahalo pia kwa wanaowania kiti cha zanzibar baina ya madevu na daktari mweupe
 
Nimekuwa nikichangishwa mambo mengi kwenye jamii na mengine hayana hata maana, sioni sababu kwa nini nisite kuchangia gharama za mdahalo utakaonisaidia kujua uwezo walionao wanaowania kuniongoza kwa miaka mitano ijayo.
Shs 100,000 zitapatikana kutoka kwa Chakaza bila shaka.
 
Kwa mtazamo wangu midahalo kama hii hutayarishwa na vituo vya TV kibiashara zaidi,
wao wanatumia muda wa prime time kwa sababu ya kutazamwa na wengi. Makampuni
yanayopenda kutangaza bidhaa zao huvutika zaidi katika vipindi kama hivyo na muda
kama huo ili bidhaa zao ziweze kufahamika na wengi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom