Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nilishuhudia mdahalo wa wagombea Urais wa TLS, uliofanyika katika kituo Cha luninga Cha Star TV, ukiongozwa na mtangazaji wao mahiri, Chifu Odemba, ulioendeshwa Kwa takribani masaa mawili na nusu, ambao ulikuwa mzuri sana na wa kiwango Cha kimataifa, ambao uligusa Kila aina ya nyanja ya taaluma hiyo ya sheria na Taifa Kwa ujumla.
Ningependelea na naamini watanzania walio wengi, ndivyo watakavyopendelea kuona mdahalo wa aina hiyo, Kwenye uchaguzi Mkuu wa mwakani wa wagombea wa vyama vya siasa mwakani, ukiendeshwa na kituo hicho, chini ya mtangazaji nguli Chifu Odemba.
Hata hivyo najua kuwa kulifanyika juhudi kubwa miaka ya nyuma, Kila ilipofika wakati wa uchaguzi mkuu, kuwataka wagombea wa vyama vya siasa, washiriki Kwenye mdahalo wa aina hiyo, lakini kizingiti kikubwa ilikuwa chama Cha CCM, ambacho kimekuwa kikiukataa mdahalo huo!
Ninaamini pia kupitia Kwenye mdahalo huo, ndipo tutawajua wagombea Urais wa vyama mbalimbali, kuhusu sera zao na namna watakavyokabiliana na uongozi na namna ya kuliletea maendeleo makubwa Taifa letu
Tutambue pia kuwa ni Karibu mataifa yote duniani, yanatumia mtindo huu wa mdahalo wa wagombea Urais, Kila inapofika nyakati za uchaguzi.
Mathalani tulishuhudia hivi karibuni huko nchini Marekani, wagombea Urais wa vyama vya Democrats, Joe Biden na mwenzske wa Republican, Donald Trump, wakichuana vikali katika mdahalo huo, ambao hatimaye umemuweka pembeni mgombea Urais wa chama Cha Democrats, Joe Biden, baada ya kufanya vibaya Kwenye mdahalo huo, sababu zikielezwa kuwa ni kutokana na umri mkubwa.
Hivi bila mdahalo huo, nchi ya Marekani ingeweza kuwa na mgombea Urais wa Chama Cha Democrats, Kamara Harris??
Jibu ni Hapana
Kwa hiyo Kwa kuwa tunajua umuhimu mkubwa wa kuwa na Rais Bora kwa Taifa lolote ni jukumu kubwa sana Kwa maendeleo ya wananchi wa Taifa husika, Kwa hiyo naamini upo ulazima wa kuendesha mdahalo wa aina hiyo, Ili tuweze kuwapima wagombea wetu wa Urais, tunaotegemea kuwapigia kura, Ili waweze kuliongoza Kwa weledi mkubwa Taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania
Pia, soma: Mdahalo wa Wagombea Urais wa Chama cha Mawakili Tanzania Bara 2024