Ally Msangi
JF-Expert Member
- Jun 29, 2010
- 608
- 120
Wagombea wa urais wote watashiriki isipokuwa yule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohamed Shein ambapo kutokushiriki kwake kunatokana na uamuzi wa chama chake kuwakataza wagombea wake kushiriki katika midahalo na kwamba, midahalo yao ni katika mikutano ya hadhara ikiwa ni pamoja na kutangaza mafanikio ya ilani ya 2005/2010 pamoja na mipango na matarajio ya mwaka 2010/2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibandamaiti, Kaimu Katibu mkuu wa CUF, Salim Bimani alisema mdahalo huo utafanyika katika ukumbi wa Bwawani, Unguja.
"Kesho (leo) wanaCUF mnatakiwa mtulizane kimya majumbani ili muweze kumsikia na kumuona vizuri Maalim Seif atakapokuwa katika mdahalo utakofanyika Bwawani,'' alisema Bimani na kuongeza kuwa Maalim Seif ataulizwa na kujibu maswali papo kwa papo kutoka ukumbini hapo na kwa njia ya simu kutoka majumbani.
Bimani ambaye pia ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi, alisema mdahalo huo utaanza saa 4:00 asubuhi. "Kutokana na mdahalo huo, kampeni za Maalim Seif zitasimama kwa leo na zitaendelea kesho kutwa,'' alisema Bimani.