Mdogo mdogo, Diamond atabwia unga

mleta mada umeeleweka Hatumuombei mabaya lakin mama ake amkalishe kitako sababu kila mchuma janga hula na wakwao!!?
 
Swadaktaaaaa.!! Well said mkuu
 
Hio ni aina ya maisha aliyoyachagua alimradi hajavunja katiba ya jamuhuri ya muungano, mbona wabongo hamuishi jealous?
Hivi ingekuwa wewe usingenunua harrier ama bmw, usingejenga nyumba kali, usingegonga watoto wakali? Yote haya ni kwa vile hujapata fursa ya kumiliki u star ulioghubikwa na pesa nyingi mno hivyo kausha kiume.
Wabongo wanakera hapo tu hebu jifunzeni hiki kitu aisee "LIBERTY"
 
Ulichokisema kinaweza kuwa ni kweli hatakiwi kuiga kila jambo linalofanywa au kulitamani toka alivyokuwa mdogo ( maana alishasema mambo mengi anayofanya aliyatamani akiwa mdogo) na hii si kwa yeye tu hata sisi wa mtaani na si mwenye pesa tu na hata hoe hae kwani kila mtu ana kiwango chake cha starehe kulingana na kipato chake. Lakini tatizo lako umeongelea kama vile unamuhisi pengine hajajiwekea limiti ya uigaji anaoufanya (umejaribu kutaja hatua za kuendelea kujaribu ) Na kwa haya unayosema Mama yake yupo makini sana naye kwenye kumtahadharisha ili asipitilize kwenye uigaji na ndio maana mpango wake wa kuendelea kujimilikisha Migari ya kifahari kauhairisha na hii ni kutokana na ushauri wa mama yake aliyemuhoji "unataka kununua magari ya ya kifahari ya milioni 500 - m600 kwanini hizo pesa usiziwekeze kwenye majumba ??" Kwa hiyo usihofu mleta mada mama yake ndio muongozo wake hatopitiliza, na uzuri ni kwamba anamsikiliza sana Mama yake, na kweli asingekuwa na yule mama pengine asingekuwepo hadi leo kwenye muziki.
 
Angalizo murua sana, hasa kwa vijana wa leo wanaopenda kuiga kila kitu hasa vya kimarekani. Msibaki tu kubeza, ipo siku twaweza anza kushangaa kila mtu haamini kama ndio yule kweli ama kalogwa. Mwenye masikio na asikie.
 
sifahamu sana tabia za diamond,ila hivi karibuni kuna siku alitembelea ofisi fulani hivi ambayo nami pia nilikuwa mgeni kama yeye.

hapo ndio nilimuona diamond kwa ukaribu zaidi. kwa hakika alonekana mchovu sana kwa maana ya kuchoka.na macho yake yalikuwa yanaonyesha kama mtu mwenye uzingizi.

nilijiuliza maswali mengi sana kuanzia uchovu wa kazi mpaka matumizi ya "bwimbwi".
 
pesa yake hajamkaba mtu kaipata kwa jasho lake wacha aitumbue ukifa kaburi hawakuwekei hata mia. Maisha yako kama upepo bana
 
Angalizo murua sana, hasa kwa vijana wa leo wanaopenda kuiga kila kitu hasa vya kimarekani. Msibaki tu kubeza, ipo siku twaweza anza kushangaa kila mtu haamini kama ndio yule kweli ama kalogwa. Mwenye masikio na asikie.

Tatizo watu mnapenda kuongea kwa hulka... Hakuna mtu anayeishi bila kuiga tamaduni za mbele, ikiwemo wewe na nywele za wazungu/plastick.. Na kwa hivo hawezi mtu akasema kwa kuwa unaiga mitindo ya nywele, basi utaiga matumizi ya dawa za kulevya na kuingiliwa kinyume na maumbile ni vitu viwili tofauti kama ilivyo kwa mtoa mada, diamond kutupia gold mwilini kuuweka mwili kistar anapokuwa kwenye spotlight ni tofauti na upuuzi alioongea mtoa mada...
 
Angalizo murua sana, hasa kwa vijana wa leo wanaopenda kuiga kila kitu hasa vya kimarekani. Msibaki tu kubeza, ipo siku twaweza anza kushangaa kila mtu haamini kama ndio yule kweli ama kalogwa. Mwenye masikio na asikie.
Hivi vitu vipo tu, vinakuja na vitapita and wala Diamond hawezi kuwa wa mwisho!

The problem we're too paranoid na vitu vidogo vidogo kuvifanya kuwa ni big issues! Hivi anayeweka meno ya dhahabu kinywani ana tofauti gani na mtu anayening'iniza grams kadhaa za madini shingoni? Tukipata jibu, tujiulize ni watu wangapi wanafanya hayo mambo na wameathirika nini?! Are just accessories...
 
Kwanza ngoja nikuambie... sometimes ni sisi(Waafrika) wenyewe tu hatujiamini! You know what, kitambo sana enzi hizo niko Chalii wa O Level nilienda bush! Enzi zile watoto wa O Level full Mlegezo! Kufika Bush, I mean Bush nakuta uncle wangu mtu mzima nae anavaa mlegezo and I don't care kama nae ilikuwa for fashion or else lakini kinachofurahisha ni kwamba nikamsikia bibi (alikuwa above 80) akiita ile style "pondomo!" Nikajiuliza huyu uncle wangu huyo mzungu kamuonea wapi akiwa kavaa pondomo! Lakini kv hatujiamini, leo hii nikivaa pondomo watu watasema nimemuiga Lil Wayne wakati hata uncle wangu asiyemjua Lil Wayne nae full pondomo! Si hivyo tu, kuna makabila kibao ya kiafrika ambayo wanaume wanatoga na kuvaa vipini lakini leo hii ukifanya utaambiwa unaiga Wamarekani!

Anyway, inawezekana ulikuwa inspired na Wanyamwezi but what's important hizo swaga kumbe hata sisi tunazo long time kitambo! Tena usije kuta wao ndo wametuiga sisi lakini kv hatujiamini na kujithamini mara zote tunadhani sisi ndo tunaiga!
 
Iko faida kubwa sana ya mtu kwenda darasani hata kama ana akili ya kawaida ya maisha
Naombea Diamond asiishie kubaya kwakwel
 

Upo sawa mkuu kuna vitu vingi tu vimetokea Afrika, maana utamaduni siku zote unamabadiliko japo sisi tumewaiga wao kwa asilimia kubwa zaidi.
 
Pamoja na mambo mengine yote Diamond ana nidhamu sana na maisha ni kati ya vijana wanaokumbuka kua wametoka kwenye umaskini
 
Grilled teeth sio tatizo wewe mwandishi LUQMAN MALOTO , tuache kuhukumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…