Nipo hapa ufaransa kwa muda wa miezi 5 sasa, leo katika pita pita zangu kwenye ofisi moja nimesikia wimbo wa mdogo mdogo wa Diamond ukipigwa kwenye simu na Mfaransa mmoja mweye asili ya Afrika. Niliposikia nikamfuata nikijua ni Mtanazania au Mwafrica mwenye kujua Kiswahili. Chambo la Kushangaza nikuwa huyu Jamaa hajui Kiswahili hata kidogo alichojibu ni kuwa I do no Swahili but I like this kind of Music kwa mimi niliyekuwa hapo nikadhani labda amebahatisha music mmoja cha ajabu huyu Jamaa ana nyimbo nyingi za Diamond maake iliyofuata ni NUMBER ONE ya Diamond na Davido.
Kilichonishangaza zaidi pia ni kuwa huyu jamaa alikuwa anaufuatisha njisi wimbo unavyoimbwa wakati hajui Kiswahili na ninauhakika hajui kiswahili maake hapa Ufaransa mpaka upate ajira ya ofisi fulani ni lazima wahakikishe Lugha yao yaani Kifaransa unakifahamu sawasawa. Wengi wa Africa walio hapa wanatoka nchi Koloni za Wafaransa hivyo hata English kwao ni shida.
Mimi kama mzalendo Mtanzania napenda kumpongeza Diamond na wasanii wengine watanzania kwa kuendelea kukitangaza Kiswahili na nchi kwa Ujumla.
Chanzo:
Mimi mwenyewe.
BUSAMUDA