Hiyo hali mara nyingi huisha baada ya miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ila wengine huendelea mpaka wanajifungua.
Zipo sababu nyingine ila mojawapo ni kutokana na ongezeko la hormone ya kike(oestrogen) hii huusika na utambuzi wa ladha wa vyakula unavyokula.
Jinsi kiwango cha oestrogen kinavyobadilika na ndo jinsi uwezo wa kuhisi ladha hubadilika.
Kula matunda kama machungwa, zabibu au kunywa juisi yake kupunguza uchungu. Jitahidi kunywa maji mengi kwa siku. Safisha kinywa chote sugua ulimi vizuri.