Mdororo au anguko la Hiphop Tanzania

Mdororo au anguko la Hiphop Tanzania

Makonyeza

Member
Joined
Feb 2, 2020
Posts
72
Reaction score
261
Mdororo au anguko la HopHop Tz!?

Kuna msemo wa waingereza wanasema,"kimya cha marafiki zangu kinanighasi zaidi ya kelele za maadui zangu".

Familia ya wanaHip Hop Tz kwa sasa wamepoa sana,wapo kimya sana kiasi kwa sisi mashabiki ni bonge la ghasia,binafsi inaniudhi.

Angalia mfano huu,juzi juzi kuna yule dogo wa Kenya ambaye kafanikiwa kuibeba na Hiphop ikambeba pale Kenya,anajiita Khaligraph Jones, huyu mwamba aliamua tu kuwazindua kutoka usingizini wanaojiona 'Magiant' wa Muziki wa Hip Hop Tz kupitia ngoma yake ya 'Bongo Fleva'.

Hapa Jones alinyoosha maelezo akawahoji ".Big Rappers mbona mna Plan Ndogo?",

na pia akakiri kwa kinywa chake

"..kusema kweli Bongo rap imeendelea, but Mnalegea..na ndo maana nawadare.."
Tena kuna mstari anahoji na kuwataja kwa majina "siku hizi hamtoi ngoma kama zamani.."
Mengi ya msingi na ya kukera yalisemwa na Khali humu kwenye ngoma hii.

Lakini ajabu na kweli kati ya Rappers wote uwajuao Tz ni mwanadada Rosalee pekee ndiye aliyesikika kumjibu Khali, tena alimpa majibu Mujarab haswa, wengine wote kimyaaaaa.

Mtanzania aliyeonesha kukerwa na Dis ya Khali alikuwa Mwijaku🤣 ambaye bahati mbaya si Mwana Hip Hop na wana Hip Hop aliowatetea wakamwangusha.

Kama haitoshi,naibu waziri Mwana FA naye akajitoa kuwachangamsha wenzake waliolala usingizi wa Pono.

FA akawachalula akijinadi kwamba wapo wasanii wengi wa Hip Hop tz na anawakubali, lakini hakuna anayeandika zaidi yake, yaani hakuna Mwana Hip Hop Tz anayeweza kubattle na yeye kwenye muziki.

Kauli hii ya kuudhi nayo ikapita na kusahaulika kimyakimya. Mheshimiwa naibu si kama alimaanisha,ilikuwa ni katika kujaribu kuwachangamsha wana tu wajitambue warudi kwenye mstari,lakini waaaaaaaaapi,Doooroo usingizi wa PONO!

HATA aliyemjibu FA hakuna kana kwamba hawakumsikia au wamekubaliana na alichokisema. Bado jamaa wamelala ilhali kumekucha

Siku za nyuma kuna mwamba aliona mbaaaali akaweka wazi kwamba HOP Hip Kibongo Bongo Bongo bora kuuza Pipi. Mtoto wa Manzese Madee kutoka familia ya TipTop alibainisha kwamba Hip Hop haiuzi.
Wakamnunia,wakamuwekea mabiff na wengine waahidi kumsaka kumshikisha adabu,lakini leo imedhihirika aliona mbali.

Hofu yangu ni kama aliyokuwa nayo Afande wa Bongo Flavor mtoto wa Morogoro,rastaman asiyefeki maisha,alihofu na kuhoji .." iko wapi Taarabu,ilikuja kwa kishindo hata wagumu walishahusudu.."

Wasipoangalia punde watajikuta kule iliko Taarabu ambayo kimsingi imeshajifia na waimbaji wake akiina Isha Mashauzi wameamua kujikita kwenye biashara za mapishi na maigizo.

Kwa sasa nawaona kwa mbaaaaali mdogo wangu Roma na Ney Wa Mitego wakijikongoja kujibebesha muziki wa Hip Hop mabegani kwake, lakini bahati mbaya sana aina ya meseji zake waanakosa airtime kwenye vyombo vya habari na kufanya jitihada zao sawa na kutwanga maji tu!

Chid Benzi ndo kama mnavyomuona, Sugu na FA mwenyewe siasa imewachukua kimoja,hawana muda na Kuandika wala kushika mic kwa sasa. FidQ kadharika naona amejikataa mwenyewe kabla ya kukataliwa licha ya kuaminjwa sana na wapenzi wa Hip Hop. Afande Sele naye yuko bize anajitafuta kwenye siasa.

Kuna kipindi miaka ya mwanzoni 2000 kila kijana alitaka kuwa mwana hiphop,hata mimi binafsi nakumbuka nilishawahi kurekodi kwa producer Kameta ngoma inaitwa Weekend🤣 nikiwa na wanangu Side Boiler na Wise Man na kundi letu la MWB Family.
Lakini si leo,bongo Hip Hop imepoteza mvuto na ushawishi,hakuna anayeitaka,kila kijana anataka kuimba na si kuchana.

Nikamkumbuka Mangwea,dah!
Kisha nikabaki najiuliza,hii ni Mdororo au ndo anguko la Jumla ya Bongo hip Hop?!

Ndimi Mwalimu wa Kiswahili,
Ukiniita Galacha wa kalamu,
nitaitika bila ya taabu
 
Hip hop inakumbana na changamoto nyingi sana sio bongo tu ni world wide hasa baada ya haya mambo ya upinde upinde kuchukua hatamu
 
Hip hop inakumbana na changamoto nyingi sana sio bongo tu ni world wide hasa baada ya haya mambo ya upinde upinde kuchukua hatamu
Jazia nyama mkuu kivipi?

Unaonekana una hoja nzito
 
Tatizo ni BEAT Na Mashahiri yakuandikia Studio. Utakuta msanii ana wimbo mmoja mreeefu anaugawa katika beat 10 akitafuta na viitikio basi anazindua album.
 
Ni aina ya walaji wa sasa. Hawa gen z wa 2000s wanatk ngoma aina za ya kina mond. Na pia mwelekeo wa nchi kisiasa pia unachangia.
 
Nimesoma maoni yako, hakuna mdororo wala anguko
Bado hiphop inafanya vizuri utofauti ni ile ngumu sana kwa sasa ni kama watu wameacha kufanya
Hiphop haiwezi kuanguka maana hayo ni maisha

Nikitulia ntaenda ile post ya freestyle michano nipige vi-bars kadhaa
 
Wakiendelea kuzingua, tunawapa genZ 👑
 
Back
Top Bottom